Tiba kwa mgonjwa wa kisukari zimegawanyika kulingana na aina ya kisukari chenyewe. Katika mada hii tutaangalia tiba kwa mgonjwa wa kisukari na jinsi mtu anavyoweza kudhibiti kisukari asipate madhara makubwa ama asipatwe kabisa na kisukari.
Tiba ya kisukari Ni Ipi?
Kwa kawaida hakuna tiba ya moja kwa moja tatizo la kisukari,Isipokuwa mgonjwa wa kisukari anaweza kufuata mwongozo sahihi wa jinsi ya kupunguza ongezeko la sukari katika mishipa ya damu. Kwa hiyo tunaposema tiba ya kisukari humaanisha udhibiti wa ongezeko la sukari na siyo kuondoa sukari kabisa katika mishipa ya damu.
Ongezeko la sukari huweza kupunguzwa kwa; Kuongeza uwezo wa kongosho kuzalisha insulini ya kutosha,Kupunguza kiwango cha glucose inayotolewa na ini,Kuongeza uwezo wa seli za mwili kupokea insulini,Kupunguza kiwango cha wanga kinachofyonzwa ndani ya utumbo mwembamba,Lakini pia kuongeza uwezo wa kumeng'enya chakula taratibu kwa muda mrefu ili kisharibiwa vyema.
Wataalamu wa afya wamegundua njia kadha wa kadha ili kuondoa madhara zaida ya tatizo la kisukari. Hapa zipo njia kadhaa kwa mgonjwa wa type 1 na type 2 diabetes.
Mgonjwa wa type 1 diabetes;
(a) Insulin ijection
Ni sindano za insulin na mgonjwa huchomwa sindano hizi wengine huhitaji mbili hadi nne kwa siku.
(b) Insulin pump therapy
Hii huwafaa sana watu wenye kiwango kidogo cha sukari (hypoglycemia). Hii ni mbadala wa sindano ya insulin. Hiki ni kifaa kidogo ukubwa wa karata hivi ambacho huwa na insulini. Insulin ndani ya kifaa hiki humfikia mgonjwa kupitia ncha ndogo ya sindano ambayo hudumbukizwa maeneo ya tumbo kwa walio wengi. Wengine hukipachika maeneo ya mapaja,matako ama mkononi.
(c) Islet cells implants
Hizi ni seli zinazozalisha insulini. Wakati fulani hubadilishwa na kuwekwa zingine ili kujaribu kuleta ufanisi wa uzalishwaji wa insulini.
Mgonjwa wa type 2 diabetes
(a) Vidonge
Vidonge vinavyoweza kutolewa kwa mgonjwa huyu ni kama,
.Metformin-hupunguza kiwango cha glucose inayotolewa na ini ndani mishipa ya damu.
-Hufanya seli za mwili kupokea insulin
.Sulphonylureas- huongeza kiwango cha insulin kinachotolewa na kongosho
.PIoglitazone-huongeza uwezo wa seli pokezi kupokea insulin
.Gliptins (DPP-4 inhibitors)- huzuia kuharibiwa kwa homoni ya asili inayoitwa GLP. Homoni hii husaidia mwili kutengeneza insulin lakini baadae huharibiwa.
.SGTL2-inhibitors- huongeza kiwango cha glucose kinachotolewa kwa njia ya mkojo
.GLP agonists-huongeza kiwango cha kuzalisha insulin
.Acarbose- hufanya chakula cha wanga ulichokula kisagwe taratibu ili kutoa glucose kidogo.
.Naeglinide & Repaglinide- husaidia kutolewa kwa insulin
(b) Upasuaji ua kupunguza uzito
Hii humsaidia mgonjwa kupuza uzito wake na hivyo kupunguza madhara zaidi ya sukari
Jinsi ya kudhibiti kisukari; Unazijua njia hizi?
Kama tulivyokwishaona hapo mwanzo,kisukari type 1 haiwezekani kudhibiti kabisa. Lakini tunaweza kudhibiti kabisa sukari type 2 na Gestational diabetes. Unaweza kujidhibiti ili kuepuka kupata kisukari kabisa lakini pia unaweza kudhibiti madhara zaidi unapokuwa umepata kisukari. Naweza kusema kuwa watu wengi wanasumbuka kwa kutojua cha kufanya wanapokuwa wamepata ugonjwa wa kisukari na wengine wanashindwa kufuata njia thabiti za kujizuia usiathiriwe na kisukari.
Zipo njia tatu madhubuti za kudhibiti tatizo la kisukari ambazo zikizifuatwa kwa uaminifu mtu aweza kujiepusha na kisukari ama kuepuka madhara zaidi unapokuwa na tatizo la kisukari. Njia hizo zimeelezewa hapa chini;
(i) Kula chakula bora chenye afya

Matumizi ya chakula bora ni msing iwa afya bora. Watu wengi hawana utamaduni wa kula ili kujenga na kulinda afya zao bali hula ili kuepuka njaa. Ili uweze kuepuka matatizo yatokanayo na mtindo wa maisha ni lazima uzingatie matumizi ya chakula bora.
Sasa ili kuepuka kupatwa na kisukari ama kupata madhara zaidi unapokuwa na kisukari, tumia chakula chenye kiwango kidogo cha sukari,mafuta kidogo na chakula chenye nyuzi nyuzi kwa wingi. Chagua chakula cha aina hii kitakufaa sana;
-Kula chakula cha nyuzinyuzi kwa wingi kama vile maharage, nafaka zisizokobolewa (ngano,nafaka),mboga za majani na matunda.
-Acha kutumia vyakula vyenye mafuta mengi kama vile; chips,crips,tambi na vinginevyo. Epuka pia matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula, wakati fulani ikikulazimu kutumia mafuta tumia haya; mafuta ya mimea,mafuta ya nazi na mafuta ya tini.
-Usile samaki na nyama zenye mafuta mengi. Epuka pia matumizi ya sausage,burgers na nyama iliyokaangwa kwa mafuta. Badala yake kula nyama iliyookwa,ama iliyochomwa kwa mvuke wa moto.
(ii) Fanya mazoezi
Mazoezi husabaisha misuli kutanuka na kutumia glucose nyingi. Misuli huihitaji insulini ili kutumia glucoes toka ndani ya mishipa ya damu. Kwa mtu yeyote asiyefanya mazoezi yuko katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa kuwa sukari itakuwa nyingi mwilini na kusababisha seli pokezi (receptor cells) za insulin kushindwa kupokea insulin (insulin resistance) na ikifikia hapa tatizo la kisukari linatokea maana sukari itakuwa nyingi na namn aya kuiondoa hatakuwepo.Lakini kwa kufanya mazoezi kiwango cha sukari kitapunguzwa sana.

Kwa mtu mwenye kisukari mazoezi yatasaidia misuli yake kupunguza sukari mwilini mwake moja kwa moja bila uhitaji wa insulini. Hapa mgonjwa wa type 1 diabetes sasa anaweza kupata ahueni kubwa kwa kuwa hana insulini kabisa. Lakini pia mgonjwa wa type 2 akifanya mazoezi atadhibiti kiasi kikubwa cha sukari kilichozidi mwilini mwake.
Kwa kawaida mazoezi yana umuhimu mkubwa katika mwili. Hapa chini kuna faida nyingine muhimu za mazoezi kwa ajili ya afya yako;
.Mazoezi hupunguza matatizo ya moyo kwa kutanua mishipa ya damu na kusaidia kuepuka tatizo la Atheriosclerosis
.Huweka kiwango takiwa cha mafuta mwilini (blood cholestrol)
.mgandamizo mkubwa wa damu (high blood pressure)
.Hufanya misuli na mifupa kuwa imara
.Husaidia kupunguza uzito wa mwili
.Huondoa msongo wa mawazo na kuleta usingizi mzuri
Lakini kabla ya kuanza mazoezi tafadhali wasiliana na daktari wako akague afya yako na kukupangia mazoezi yanayokustahili. Unaweza kuanza mazoezi pasipo kufanya vipimo na ukapata shida baadaye.
(iii) Punguza uzito wako
Mtu mwenye uzito mkubwa yuko katika hatari kubwa sana ya kupata ugonjwa wa kisukari. Kupunguza uzito kwa kiwango cha 5% huweza kupunguza hatari ya kupata tatizo la sukari kwa zaidi ya 50%. Hapa unaweza kuona umuhimu mkubwa wa kupunguza uzito ili kuepuka hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu hasa type 2 na gestational diabetes.
Njia nyingine za kupunguza hatari ya kisukari;
-Epuka kuvuta sigara
-Punguza unywaji wa pombe
-Pata chanjo ama sindano ya insulini
-Tunza miguu yako kwa tahadhari,kata kucha,safisha miguu na pia vaa viatu.
-Fanya uchunguzi wa mara kwa mara wa macho yako.
-Dhibiti high blood pressure
-Dhibiti kiwango cha cholestrol mwilini
-Epukana na msongo wa mawazo
Asante kwa kuungana nasi katika mada hii ya kisukari. Imekuwa mada ndefu,lakini umuhimu wake umekuwa kukuonesha chanzo cha kisukari,dalili na madhara ya kisukari na hatimaye tiba na jinsi ya kudhibiti kisukari.
Kama unasumbukana tatizo hili tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959.
Usisite kuuliza swali ama kutoa maoni kuhusiana na mada hii.

