UVIMBE WA TEZI DUME-BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH)

Tezi dume (prostate gland)  ni tezi inayopatikana kwa wanaume yenye ukubwa kama karanga kubwa. Tezi hii hupatikana chini kidogo ya kib... thumbnail 1 summary




Tezi dume (prostate gland)  ni tezi inayopatikana kwa wanaume yenye ukubwa kama karanga kubwa. Tezi hii hupatikana chini kidogo ya kibofu cha mkojo mbele ya njia ya haja kubwa (rectum). Tezi hii hutengeneza maji maji muhimu (prostate fluids) ambayo husaidia kurutubisha na kulinda mbegu za kiume. Lakini pia misuli ya tezi hii husaidia kusukuma mchanganyiko wa mbegu za kiume kwa nguvu. Mwanaume anapofikia miaka 40 tezi hii huanza kuvimba na kuongezeka ukubwa,japo matatizo mengi ya tezi hii huonekana kwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 60. Hali hii huitwa Benign Prostatic Hyperplasia (BPH). Tezi dume hupatikana chini kidogo ya kibofu cha mkojo,kuzunguka mrija wa urethra unaopitisha mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu cha mkojo. Tezi hii ikiendelea kukua,hubana mrija wa urethra na kusababisha maumivu makali wakati wa kukojoa.




Chanzo cha Tezi Dume Kuvimba






Chanzo cha uvimbe huu wa tezi bado hakijulikani vyema. Lakini inaaminika kuwa uvimbe weweza kuchangiwa na uwepo wa korodani na umri kuongezeka. Kwa wanaume waliowahi kufanyiwa upasuaji wa kuondoa korodani katika umri mdogo, hawawezi kabisa kupata tatizo hili la tezi kuvimba. Kwa kadri umri unavyoongezeka mabadiliko ya homoni ya testesterone hutokea. Haya mabadiliko ya homoni huweza kusababisha seli kuongezeka. Seli zikiongezeka  husababisha tezi ya kiume kuongezeka na kuwa kubwa kuliko kawaida. Lakini ufahamu ndugu msomaji kuwa kuvimba kwa tezi dume huku sio kansa kwa sababu hakuenei sehemu zingine za mwili,bali ni uvimbe tu (benign)





Dalili na Madhara ya Tezi Ya Kiume Kuvimba





Dalili hizi katika hatua za mwanzo zimefichika sana ila zitachachamaa kama tatizo halitatibiwa kwa muda mrefu. Dalili hizo ni kama zifuatazo;

-Kibofu kujaa muda wote
-Kuamka mara kwa mara usiku kukojoa (noturia)
-Kushindwa kuzuia mkojo
-Kukojoa mkojo dhaifu
-Kujisikia unataka kukojoa muda wote
-Maumivu wakati wa kukojoa
-Kukojoa mkojo wenye damu
-Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
-Kupata shida wakati unaanza kukojoa



Madhara ya kuwa na uvimbe wa tezi dume kwa muda mrefu ni kama yafuatayo;

-Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTIs)
-Matatizo ya figo (kidney damage)
-Mawe kwenye kibofu cha mkojo (bladder stones)
-Kutokwa damu kwenye mfumo wa mkojo
-Kushindwa kutoa mkojo



Tiba ya Uvimbe wa tezi dume





Tiba ya uvimbe huu huanza na uangalizi binafsi. Kama dalili hazitadhibitiwa kwa tahadhali binafsi,basi utatakiwa kufanyiwa upasuaji. Lakini pia umri wako na hatua ya ugonjwa ndio itapendekeza aina ya tiba utakayotakiwa kupatiwa. Tahadhali binafsi yaweza kuhusisha;





-Kojoa kila mara utakapohisi hitaji la kufanyahivyo,usibane mkojo

-Jenga mazoea ya kwenda chooni kukojoa hata kama huhisi haja ya mkojo

-Epuka kunywa pombe

-Epuka matumizi ya caffeine

-Epuka msongo wa mawazo ili kuepuka mkojo mwingi kutengenezwa

-Fanya mazoezi mara kwa mara,kutofanya mazoezi kutasababisha madhara zaidi

-Fanya mazoezi ya kegel kuimarisha misuli yako

-Epuka ubaridi maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi

Tiba nyingine zaweza kuwa:

Alfa-1 blockers- Ni dawa zinazotanua misuli ya shingo ya kibofu na tezi ili kufanya mkojo utoke kwa urahisi. Dawa hizi ni kama zifuatazo; tamsulosin,terazosin,alfuzosin,prazosin,doxazosin

Homonal reduction-Dawa kama dutasteride na finasteride hutolewa na madaktari ili kupunguza kiwango cha testesterone. Kupunguzwa kwa testerone huweza kupunguza ukubwa wa uvimbe wa tezi hii. Lakini dawa hizi pia zina madara kama kusababisha ugumba kwa mwanaume na kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Antibiotics- kama uvimbe utakuwa umedumu kwa muda mrefu na kusababisha maambukizi ya tezi dume,basi dawa hizi daktari atakuandikia ili kupunguza maambukizi.

BPH surgery- Wakati fulani utalazimika kufanyiwa upasuaji,japo kwa baadhi ya watu madhara zaidi huonekana kutokana na upasuaji. Madhara kama mkojo kutoka moja kwa moja na mbegu za kiume kutoka pia.

Madaktari watakufanyia upasuaji kama tezi dume itakuwa imekusababishia moja ya matatizo haya;

-Kidney failure
-Mawe kwenye kibofu cha mkojo
-Urine Tract Infections (UTI)
-Kutozuia mkojo (urine incontinence)
-Kibofu kujaa muda wote
-Damu kwenye mkojo kwa muda mrefu



Leo tutashia hapa kwenye mada hii ya Uvimbe wa Tezi dume. Naamini umepata elimu ya kutosha kukufahamisha tezi dume ni nini na kwa nini inavimba na tahadhali unazoweza kuchukua kuepuka madhara zaidi. Katika mada zitakazofuata tutatazama maambukizi ya tezi dume na
kansa ya tezi dume. Endelea kuwa nasi.


Kama una tatizo hili,ama unakabiliwa na moja ya madhara tuliyoyaona hapo juu, wasiliana nasi kupata tiba bora ya Tezi Dume kabla hujapata madhara zaidi. Tupigie simu 0673 923 959.

Kama una swali,maoni au ushauri usisite kutuandikia,nasi tutakuhudumia maana ni furaha yetu.