UNENE KUPITA KIASI (OBESITY) NI NINI?

Unene kupita kiasi (Obesity) ni kuongezeka kwa mafuta mwilini kupita kiasi ambayo huweza kusababisha madhara mwilini. Unene kupit... thumbnail 1 summary








Unene kupita kiasi (Obesity) ni kuongezeka kwa mafuta mwilini kupita kiasi ambayo huweza kusababisha madhara mwilini. Unene kupita kiasi husababishwa na kuingiza mwilini nishati kuliko kiwango kinachotakiwa na mwili.

Mwili wako huhitaji nishati kukusaidia kuwa kuishi na kusaidia utendaji kazi wa viungo vyote vya mwili wako. Nishati huongezeka mwilini kila mara unapokula au kunywa. Mwili wako hutumia nishati kila siku katika utendaji kazi wa mwili kama vile upumuaji,kutembea au kukimbia.

Ili kuwa na uzito na unene unaotakiwa,nishati unayoingiza mwilini inatakiwa kuwa sawa na nishati inayotumiwa na mwili. Kama unahitaji kupunguza uzito au unene wako basi huna budi kumudu nishati unayoingiza mwilini na nishati inayotumiwa na mwili wako.



Utajuaje Kama Una Unene Au Uzito Uliopitiliza?



Nadhani umekuwa ukijiliza swali hili,nitajuaje kuwa nina tatizo la unene au uzito kupita kiasi? Ndiyo ni muhimu ujue kama una tatizo ili uanze kwa haraka mpango wa kupunguza na kuepukan ana tatizo tena. Japo vipo vipimo vingi,kipimo rahisi cha BMI (Body Mass Index) kimekuwa kikitumika kubainisha kama una tatizo la uzito au unene kupita kiasi.

BMI ni kipimo cha mafuta yaliyo mwilini kwa kikihusisha uwiano wa uzito na urefu wa kimo chako. Mara nyingi hutumika kwa watu wenye umri wa miaka 20 na kuendelea. Kipimo hiki kilianzishwa na mwanahisabati,mnajimu na mwanatakwimu mbeligiji aliyeitwa Adolphe Quetelet mwaka 1832 wakati huo kikiitwa Quetelet Index. Baadaye kiliitwa Body Mass Index mwaka 1972 na Ancel Keys.

Kanuni ya BMI ni kuganya uzito wako (kilogram) kwa namba mraba ya urefu wako (mita). Kwa mfano kama uzito wako ni kg 65 na urefu wako ni sentimita 150,basi BMI yako ni:

65kg/150cm=65kg/1.5mx1.5m


Hivyo BMI yako ni 65kg/2.25m=28.9


Maelezo muhimu:


.BMI ya 18.5 hadi 24.9 inaonesha kuwa una uzito wa kawaida (normal weight)

.BMI ya 25 hadi 29.9 inaonyesha kuwa una Uzito kupita kiasi (overweight)

.BMI ya 30 na kuendelea ni Unene kupita kiasi (Obesity)


Chanzo Cha Kuwa Na Unene Kupita Kiasi







Unene kupita kiasi husababishwa na nini? Hapa kuna sababu zinazoweza kusababisha mtu kuwa na unene kupita kiasi:


Kalori

Hiki ni kiwango cha nishati katika chakula unachokula. Mwanaume huhitaji kiasi cha kalori 2500 kwa siku ili kuwa na uzito au unene sahihi na mwanamke huhitaji kiasi cha kalori 2000 kwa siku ili kuwa na uzito na unene usiopitiliza.
Kula chakula chenye kalori nyingi kwa wingi na kukosa mazoezi ya viungo ni sababu kubwa ya kuwa mnene kupita kiasi.

Ulaji dhaifu

Unene kupita kiasi si jambo linaloweza kutokea ndani ya usiku mmoja tu. Ni matokeo ya siku nyingi ya ulaji dhaifu na mtindo mbaya w amaisha kama:

-Kula vyakula vya kusindikwa kwa wingi ambavyo vinaweza kuwa na mafuta na sukari nyingi

-Kunywa pombe kwa wingi-pombe kwa kawaid aina kalori nyingi sana na watu wanaokunywa mara nyingi huwa wanene kupita kiasi

-Kula chakula kingi chenye mafuta mengi mara kwa mara

-Kunywa vinywaji vyenye sukari kwa wingi kama vile vinywaji laini na juisi

-Kula kupita kiasi-hii huweza kutokea unapokuwa na msongo na unaona bora ujifariji kwa kula sana au utakapohitaji kumridhisha mtu fulani.

Kwa namna fulani tabia ya kula huweza kurithiwa katika familia. Unaweza kujifunza tabia mbaya ya kula unapokuwa mdogo na ukaiendeleza hata utu uzimw wako.

Kukosa Mazoezi ya mwili

Hii ni aina nyingine ya sababu inayochangia kw anguvu sana tatizo la kuw ana unene mkubwa kupita kiasi. Ukikosa mazoezi hutaweza kutumia nishati iliyoingia mwilini kupitia chakula ulichokula. Hivyo nishati ya ziada itatunzwa mwilini kama mafuta. Watu wengi kwa sababu ya kazi walizo nazo maofisini ni watu wa kukaa muda mrefu na baada ya hapo hupanda gari na kukaa tena. Hawana mazoezi hata kwa njia ya kutembe aau kukimbia. HIyo ni hatari.


Sababu Za Kinasaba


Kwa baadhi ya watu kuna tabia ya kurithi tabia fulani zinazoweza kusababisha unene. Kwa mfano mtu aweza kurithi hali ya kupenda kula sana,kweli hii itamfanya awe mnene kupita kiasi tu. Lakini mtu yeyote mwenye kudhamiria kupunguza uzito au unene wake anaweza.


Matumizi ya madawa

Kutumia dawa za kupunguza msongo na mfadhaiko huweza kusababisha ongezeko la uzito na unene kupita kiasi.

Kuacha ghafula kuvuta Sigara

Mtu anayevuta sigara na kuacha ghafla,ile hamu na kiu ya sigara huweza kusababisha uzito wake kuongezeka kupita kiasi kwa haraka.



Mada itakayofuata tutatazama Madhara ya Unene Kupita Kiasi. Tafadhali endelea kuwa nasi.


Je,una swali,maoni au ushauri kuhusiana na mada hii? Tuandikie kupitia maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959. Ni furaha kusikia toka kwako pia.

No comments

Post a Comment