KANSA YA TEZI DUME-PROSTATE CANCER

Saratani ya tezi dume ni ugonjwa unaowapata wanaume tu. Hutokana na uvimbe wa tezi dume. Uvimbe huu huanzia ndani ya tezi yenyew... thumbnail 1 summary








Saratani ya tezi dume ni ugonjwa unaowapata wanaume tu. Hutokana na uvimbe wa tezi dume. Uvimbe huu huanzia ndani ya tezi yenyewe na kuenea sehemu nyingine za mwili. Siyo kila uvimbe wa tezi dume ni kansa bali ni uvimbe unaoanzia pale kwenye tezi na kuenea sehemu nyingine za mwili. Kwa kawaida kansa hutokea pale seli za mwili zinapojizalisha na kuongezeka bila kizuizi kwa namna isiyo ya kawaida.
Kansa hii huweza kuenea kwa taratibu kwa baadhi ya watu na kwa wengine huweza huenea kwa haraka zaidi. Uwezekano wa kupata kansa hii huongezeka kwa kadri umri unavyoongezeka. Wanaume wenye umri wa miaka zaidi ya 60 ndio huwa katika hatari kubwa ya kupatwa na aina hii ya ugonjwa. Kama kansa hii itagungulika ikiwa ndani ya tezi yenyewe ni rahisi sana kutibika na kuidhibiti kabisa kwa urahisi.


Chanzo Cha Saratani Ya Tezi Dume




Hakuna chanzo kinachojulikana cha kansa hii ya tezi ya kiume.Madaktari wanakubaliana kuwa hakuna chanzo cha ugonjwa huu kimekwishabainishwa hadi sasa. Inafahamika tu kwamba kansa hii hutokana na kukua na kuongezeka kwa seli za tezi hii ya kiume kwa namna isiyo ya kawaida. Kwa kadri seli hizi za kansa zinavyoongezeka hujikusanya na kutengeneza uvimbe (tumor). Seli hizi za kansa zilizotengeneza uvimbe huendelea kuongezeka na kugawanyika na hatimaye huanza kuenea sehemu zingine za mwili. Japo haifahamiki vyema sababu ya uvimbe huu kutokea,kuna sababu hatarishi au sababu sababishi za kutokea kwa saratani hii. Hebu tuzitazame;

Umri mkubwa- uwezekano wa kupata saratani hii huongezeka kwa kadri umri unavyoongezeka. Kwa wanaume wenye miaka 50 au zaidi huwa katika hatari kubwa ya kupata kansa hii. Lakini zaidi ya 60% ya matatizo yote ya kansa ya tezi ya kiume huwapata wanawake wenye umri wa 65 au zaidi.

Historia ya familia- kama unatokea kwenye familia yenye historia ya ugonjwa huu,mfano baba au kaka akiwa na ugonjwa huu,uwezekano wa kupatwa na saratani hii ni mara mbili zaidi.

Rangi au asili- Wamarekani wenye asili ya Afrika,Wajamaika wenye asili ya Afrika na Waafrika wenyewe wana hatari kubwa ya kupatwa na aina hii ya kansa ya kiume. Watu wa Asia na Hispania kwa upande wao hawako katika hatari hii.

Unene uliopindukia- Watu wanene sana pia wako katika hatari ya kuud=gua ugonjwa huu wa kansa kuliko watu wenye miili ya kawaida na wasiokuwa na unene mkubwa.









Chakula- Ulaji wa vyakula vya nyama hasa nyekundu na mafuta kwa wingi hukuweka katika hatari kubwa ya kukumbwa na kansa hii. Kwwa upande mwingine,kutumia matunda na mboga za majani kwa wingi hupunguza hatari yako kupatwa na ugonjwa huu. Tafiti zimeonesha kuwa kutumia vyakula vyenye lycopenes kama vile nyanya zilizopikwa,madini ya selenium na matikiti husaidia kupunguza hatari ya kuugua kansa hii ya tezi ya kiume.

Mazoezi- wanume walio na ratiba nzuri ya mazoezi,huwa katikahatari ndogo sana kuliko wanaume wasiofanya mazoezi kabisa.
Magonjwa ya zinaa- kama umewahi kuumwa kisonono,uwezekano wako kupatwa na kansa hii ni mkubwa kuliko mtu ambaye hajaumwa kabisa.

Madawa- kutumia dawa za kuzuia cholestrol mwilini kama vile statins huweza kusaidia kupunguza hatari ya kupatwa na kansa hii ya kiume.



Dalili za Kansa ya Tezi Dume




Miongoni mwa magonjwa yasiyoonesha dalili mapema ni saratani ya tezi dume.  Dalili zake zimefichika sana na mara nyingi utahisi dalili itakapofikia kugandamiza mrija wa urethra. Ila ukiwa na utaratibu wa kupima mara kwa mara utaweza kujiweka katika hali nzurimapema kukabili tatizo hili. Hebu tuangalie baadhi ya dalili hapa;

-Kukojoa mkojo wenye damu
-Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
-Kukojoa mara kwa mara
-Kupata shida wakati wa kukojoa
-Kukojoa mkojo dhaifu
-Kuhisi kibofu kimejaa tu mud awote
-Kuhisi maumivu makali wakati wa kumaliza kilele cha mlima-wakati wa kutoa mbegu
-Kupata shida ya kuw amwanajeshi imara-erectile dysfunction
-Kuamka usingizini usiku kukojoa

Kama tatizo limekuwa kubwa dalili hizi zaweza kuonekena;

-Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo ,kiuno na mbavu
-Miguu kuwa dhaifu na kukosa nguvu kabisa
-Kushindwa kuzuia mkojo pindi uanzapo kukojoa
-Kushindwa kuzuia haja kubwa,gesi na vinyesi vya maji maji kwa njia ya haja kubwa.




Madhara ya Kansa ta Tezi Dume




Kansa kuenea- Kansa hii huweza kuenea kwenye viungo vingine kama vile kibofu cha mkojo,mifupa au sehemu nyinginezo. Kansa hii kwenye mifupa huweza kusababisha maumivu makali na pengine hupelekea mifupa kuvunjika. Hata kama itakuwa imesambaa kwenye viungo vingi vya mwili kansa ya tezi dume yaweza kuzuiwa kuleta madhara zaidi,japo haiwezi kutibika kabisa.

Kushindwa kuzuia mkojo au haja-kansa hii au tiba yake huweza kusababisha tatizo hili. Lakini huweza kutibika kwa kutegemea ain ayake na muda tatizo lilipodumu.

Kushindwa kuwa mwanajeshi imara- hii pia huweza kutokana na tatizo lenyewe la kansa au tiba uliyopata. Tiba hii huweza kuwa upasuaji,mionzi au tiba ya homoni. Pia hili nalo laweza kutibiwa kwa kutegemea hatua iliyofikiwa.




Jinsi Ya Kudhibiti Na Kujikinga Saratani ya Tezi Dume




Saratani hii waweza kuiepuka. Sasa hebu tutazame mambo unayoweza kufanya kuiepuka saratani hii;


Kula matunda na mboga kwa wingi- hivi hukuongezea antioxidant kwa wingi kusaidia kuondoa radikali huru mwilini mwako.

Kula chakula chenye virutubisho- hiki kitakuongezea madini na vitamini muhimu kukuwezesha kuboresha afya yako.








Fanya mazoezi- mazoezi huimarisha afya ya mwili wako  kwa ujumla. Mazoezi pia hukusaidia kupunguza uzito wako na kupunguza kiwango cha PSA tofauti na wanaume wasiofanya mazoezi ambao huwa na kiwango kikubwa cha PSA.

Punguza uzito wako- Kama una uzito mkubwa basi jitahidi sana kuupunguza na kama una uzito wa kawaida jitahidi kuudumisha. Hii itakusaidia kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa huu.

Fanya uchunguzi wa mara kwa mara-tungeweza kusema ukae hadi miaka 60 ndipo ufanye uchunguzi wa afya,lakini kwa sababu ya mtindo wa maisha ni muhimu kufanya uchunguziwa aknsa hii kuaanzia miaka 40.



Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Tezi Dume





Hakuna kipimo cha moja kwa moja cha kufanyia uchunguzi wa kansa hii. Ili kujua kam auna tatizo hili daktari wako atafanya ulinganifu wa vipimo vifuatavyo ili kujua kama unasumbuliwa na tatizo hili au hapana. Vipimo ni kama hivi;


PSA

Hii ni protein inayotengenezwa na tezi dume. Kila mwanaume ana kiasi fulani cha protein hii ambayo huongezeka kwa kadri umri unavyoongezeka. Kansa ya tezi dume huongeza utengenezwaji wa PSA. Kuongezeka kwa kiwango cha PSA kwenye damu huwa ni kiashiria kuwa mtu huyu ana kansa hii. Hata hivyo hiki si kipomo sahihi kabisa cha kansa ya tezi ya kiume. Hii ni kwa sababu zaidi ya 65% ya wanaume wenye kiwango kikubwa cha PSA hawana kansa.


Digital Rectal Examination (DRE)


Kwa kuwa tezi hii iko karibu sana na njia ya haja kubwa,daktari ataingiza kidole laini sehemu ya haja kubwa na kupapasa kuona kama tezi imeongezeka na kubadilika. Hata hivyo kwa wengi unaweza ukuta tezi haijabadilika na hivyo matokeo sahihi hayatapatikana.


Biopsy


Hapa kinyama kutokea sehemu yenye kansa huchukuliwa ili ikachunguzwe. Inaweza kuwa na uhakika kwa namna fulani japo wakati inaweza isitoe majibu sahihi kutegemeana na mahali sampuli ilipochukuliwa.


Tiba ya kansa ya tezi dume kwa upande mwingine,huweza kufanyika katika moja wpo kati ya;
-Upasuaji
-Mionzi
-Chemotherapy


Ndugu msomaji,umefanikiwa kujifunza mengi kuhusu kansa ya tezi dume. Huenda ukawa na swali au ukawa unahitaji msaada kutokana na mada hii. Hapo chini kuna mawasiliano unaweza kuwasiliana nasi.

Ktika mada iliyopita tulifanikiwa kutazama uvimbe wa tezi dume. Na katika mada itakayofuata tutatazama Maambukizi ya tezi dume. Tafadhali endelea kuungana nasi katika mfululizo wa mada zetu.

Kwa msaada zaidi,swali ama ushauri,tafadhali wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959.