Ndugu msomaji wangu,karibu katika mada hii muhimu. Kama kuna wakati ulihitaji kujua juu ya hatari itokanayo na kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni na ukakosa majibu,leo utayapata katika mada hii. Kwa kuanza fahamu kuwa kuna kutokwa na maji maji kuliko kwa kawaida na kusiko kwa kawaida kabisa.
Tezi zilizo ukeni na kwenye mlango wa kizazi hutengeneza maji maji. Majimaji haya hutiririka kila siku na kutoka nje ya mwili. Majimaji toka ukeni huchukua seli zilizokufa na bacteria na kuzitoa nje ya mwili kila siku. Hii ni njia mojawapo ya kusafisha na kutunza via vyako vya uzazi kila siku. Yanaweza kuwa maji maji yasiyo na rangi au yenye rangi ya maziwa lakini yasiyo na harufu yoyote.
Kiwango na rangi ya maji maji yatokayo ukeni hutofautiana kulingana na mzunguko wako wa kila mwezi.Ukiwa na hisia za kufanya mapenzi maji maji mazito hivi hutoka. Lakini pia wakati unanyonyesha na wakati wa hedhi kiwango na rangi huweza kuwa tofauti.
Aina Ya Maambukizi Na Uchafu Unaotoka Ukeni
Kuna aina kadhaa za uchafu unaotoka ukeni. Hapa tutatazama aina chache kama zifuatavyo:
(i) Yeast Infections (Maambukizi ya Fungus)
Yeast ni moja ya wadudu wanaopatiakana katika kundi la fungus. Kwa kawaida fungus kidogo tu hufaa kwa ajili ya afya ya via vya mwanamke. Maambukizi ya yeast husababishwa na ongezeko la fungus aina ya Candida albicans ukeni.
Chanzo Cha Maambukizi Ya Fungus Ukeni
.Kutumia Antibiotics mara kwa mara hupunguza bacteria wazuri ukeni
.Kuwa na sukari huwafanya wadudu wabaya wazidi kuzaliana kwa kuwa hupenda mazingira yenye sukari kwa wingi
.Kuwa mjamzito
.Kuwa na upungufu wa kinga mwilini
.Kukosa lishe bora
.Kuwa na tatizo la kuvurugika kwa homoni wakati wa hedhi
.Kuwa na Msongo wa Mawazo
.Kukosa usingizi wa kutosha
Wanawake walio na hatari ya kupata maambukizi ya fungus ni wale:
-Wanaotumia antibiotic kwa wingi
-Wajawazito
.Kutumia sabuni na marashi ukeni
.Kuingiza vidole ukeni kujisafisha na kujipulizia marashi
.Kutumia vidonge vya uzazi wa mpango
.Kutumia dawa za kushusha kinga
.Kupata tiba ya mionzi (Chemotherapy)
.Kuvaa nguo za kubana mara kwa mara
.Kujifuta kwa kutumia wiper
.Kutumia madawa ya kupunguza maumbile ya uke
-Wanaokuwa wameamshwa kihisia na kukaa na unyevunyevu kwa muda mrefu. Wakati mwingine wanawake walio wengi hupata maambukizi ya fungus bila sababu.
Dalili za maambukizi ya fungus ni kama:
-Kupata miwasho sehemu za nje za uke (vulva)
-Maumivu wakati wa kukojoa na wakati wa tendo la ndoa
-Kuvimba kwa kuta za uke
-Kupata vipele,makovu na rangi nyekundu kuonekana kwenye kuta za uke
-Kutokwa na uchafu mweupe mzito kama jibini ukeni.
(ii) Bacterial Vaginosis
Ni maambukizi yanatokana na kukosa uwiano wa kiukuaji kati ya bacteria wazuri wanaopatikana ukeni. Haijulikani bayana kwa nini tatizo hili hutokea. Maambukizi haya hayaenei kwa njia ya kujamiiana kabisa. Dalili za mwanamke mwenye aina ya tatizo hili ni:
-Kutokwa na uchafu mweupe,njano,kijani au wa rangi ya kijivu
-Kutokwa na harufu ya samaki ikiambatana na uchafu
-Kutokwa na uchafu mwingi baada ya tendo la ndoa
(iii) Trichomoniasis
Husababishwa na wadudu (parasite) aina ya protozoa wanaoitwa trichomonas vaginalis. Maambukizi haya huenezwa kwa njia ya kujamiiana.Karibu asilimia 70 ya wanawake na wanaume wote walio na maambukizi ya bacteria hawa huwa hawaonyeshi dalili kabisa. Lakini endapo dalili zitaonekana zitakuwa kama hizi:

-Kuwasha sehemu za ukeni
-Makovu na wekundu maeneo kuta za ukeni
-Maumivu wakati wa kukojoa
-Kutokwa na uchafu mwembamba mweupe kama mapovu wa njano au kijani wenye harufu isiyo ya kawaida kama ya samaki.
(iv) Gonorrhea (Kisonono)
Ni moja ya magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya ngono zembe. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Miongoni mwa dalili zake ni:
-Kutokwa na uchafu wa rangi ya mawingu au njano ukeni
-Kutokwa na mkojo bila kukusudia
-Kutokwa na damu katikati ya siku zake
-Kupatwa na maumivu ya nyonga.
(v) Chlamydia
Ni moja ya magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya ngono. Maambukizi haya husababishwa na bacteria wanaoitwa Chlamydia trachomatis. Japo mwanamke aliyeathirika aweza asioneshe dalili katika hatua za mwanzo na kukufanya usiwe na shaka.Huweza kuenea kupitia ngono kupitia sehemu ya kutolea haja kubwa,mdomoni au bila kondomu na mwanamme mwenye maambukizi.
Dalili zake huweza kuwa:
-Maumivu wakati wa kukojoa
-Kutokwa na uchafu wa rangi ya njano au kijani ukeni
-Maumivu chini ya tumbo
-Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Kwa mwanaume atatokwa na uchafu wa rangi ya njano au kijani ndani ya uume na korodani zitakuwa zinauma.
Madhara yake kwa mwanamke ni pamoja na kupata maambukizi ya PID,kukosa uwezo wa kuzaa watoto kama halitatibiwa kwa muda mrefu,kuzaa watoto wenye maambukizi kama mwathrika ni mama mjamzito,au kumsababishia mtoto maambukizi ya macho na Pnemonia.
Habari nzuri ni kwamba maambukizi haya yanatibika.
Jinsi Ya Kudhibiti Maambukizi Na Uchafu Kutoka Ukeni
.Unapojisafisha epuka kuingiza vidole ukeni. Hii ni kwa sababu ndani ya uke kuna tezi zinazotoa maji maji yanayofanya kazi ya kusafisha ndani. Unapoingiza vidole vyako unaingiza bacteria na maambukizi hayatakuisha.
.Epuka kujipulizia marashi ukeni
.Tumia nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba.Hizi huruhusu sehemu zako za siri kupumua.Epuka kulala na nguo za ndani usiku.
.Vaa nguo pana zisizobana mwili wako
.Kula chakula chenye lishe na virutubisho bora
.Vaa nguo kavu zisizo na unyevunyevu
.Usijisafishe ukeni kwa maji ya moto
.Osha nguo zako za ndani kwa maji ya moto kama ukiweza
.Unapojisafisha anzia mbele kurudi nyuma ili kuepuka bacteria kutoka maeneo ya haja kubwa kuingia ukeni
.Epuka kufanya ngono isiyo salama
Tumetazama kwa kina aina ya maambukizi na uchafu unaoweza kutoka ukeni. Natumai mada hii imekuwa msaada kwako. Kama una swali,maoni au ushauri usisite kutwandikia,ni furaha yetu kujumuika nawe.
Ndugu msomaji una tatizo la Maambukizi au kutokwa na uchafu ukeni mara kwa mara? Tuna tiba mahususi na bora kwa ajili yako. Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu 0673 923 959 au barua pepe maishaniafya@gmail.com





No comments
Post a Comment