Utangulizi
ya Imarisha Afya Yako.
Tovuti yetu ni tovuti inayokupa fursa ya kipekee wewe mtanzania unayezungumza kiswahili,kujifunza na kufahamu magonjwa mbali mbali na jinsi unavyoweza kupata tiba yake. Najua kuna wengi wanaotafuta kujua tabia,chanzo,madhara na tiba ya magonjwa kadha wa kadha yaliyo tishio kwa jamii leo. Katika tovuti hii,tutatazama magonjwa mengi yaliyo tishio katika jamii na jinsi ya kuyaepuka,kuyatibu na kuondokana nayo katika jamii yetu.
Utakubaliana nami ndugu msomaji kuwa afya ndio mhimili wa maendeleo yoyote na ufanisi wowote anaoweza kuufikia mtu yeyote. Hivyo kwa kuutambua umuhimu huo,tumeona tuiandike tovuti hii kukusaidia wewe Mtanzania wa kawaida kabisa uweze kusoma na kuelewa kwa ufasaha kabisa njia bora za kupata tiba sahihi kwa ajili ya matatizo yakusumbuayo.
Kumekuwa na matatizo mengi sana ya kiafya katika jamii yetu na maelfu wamekuwa wakisumbuka kwa kukosa msaada pindi wakabiliwapo na majanga mazito ya kiafya. Kupitia tovuti hii utapata maelezo ya kina kukusaidia wewe kuelewa sababu za tatizo na ufumbuzi yakinifu wa tatizo ni upi kama utakuwa unakabiliwa na tatizo lolote ili kuepuka madhara zaidi.Hapa pia utapata ushauri juu ya tiba bora na zisizo na madhara ya kikemikali kabisa.
Mpangilio Wa Tovuti
Tumepanga tovuti hii kufuatana na matatizo yaliyopo katika jamii. Magonjwa yote ya akina mama tumeyaweka kwenye kundi moja. Matatizo kama Mwanamke Kukosa Mtoto-Ugumba,Kansa Ya Shingo Ya Kizazi-Cervical Cancer,Uvimbe Kwenye Mfuko Wa Uzazi-Fibroids,
Maumivu Kabla Ya Hedhi na Maumivu Wakati Wa Hedhi,Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa na mengine mengi.
Lakini pia kuna kundi la magonjwa na matatizo ya wanaume. Haya tumeyaweka kwenye kundi la Magonjwa Ya Wanaume. Magonjwa kama Uvimbe Wa Tezi Dume,Kansa Ya Tezi Dume,Kuwahi Kufika Kileleni, Jogoo Kushindwa Kuwika na mengine mengi.
Kuna kudi jingine la magonjwa mchanganyiko. Haya ni magonjwa yaliyojaa kila kona ya jamii. Magonjwa kama High blood pressure,Unene Uliopitiliza,Msongo Wa Mawazo,
Vidonda Vya Tumbo,Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo,Magonjwa Ya Mifupa,
Magonjwa Ya Arthritis,Ugonjwa Wa Kisukari na mengine mengi.
Kuna mpangilio mwingine unaohusiana na kupunguza unene,ambapo tumejadili hatari za unene kuongezeka kupita kiasi na jinsi utakavyoweza kupunguza unene wako.
Lakini pia kuna namna ya kufanya mawasiliano nasi kupitia fomu ya mawasiliano,na mpangilio wa mwisho ni kuhusiana na privacy policy.
Dawa Zetu
Dawa zetu ni virutubisho kwa asili,zilizotengenezwa kutokana na mimea asilia na madini muhimu kwa ajili ya afya ya binadamu. Dawa hizi hazina kemikali kabisa. Umuhimu na ubora wa bidhaa hizi umezidi kuonekana siku kwa siku kwa sababu ya uwezo wake wa kudhibiti na kuondoa chanzo cha tatizo. Dawa hizi hazishughulikii tatizo tu na kuacah chanzo,maana ukiondoa tatizo bila kung'oa mzizi (chanzo) cha tatizo,tatizo litaendelea kuwepo,laweza kutulia kwa muda mfupi lakini baadaye linaweza kurudia. Badala yake hizi hung'oa chanzo cha tatizo na hivyo kuondoa tatizo kwa ujumla wake.
Kwa tatizo lolote lenye chanzo bayana na kilichothibitishwa,basi fahamu kuwa hili linaweza kupona na kudhibitiwa kwa kutumia dawa hizi. Hii ni kwa sababu zitafanya kazi ya kuondoa na kudhibiti chanzo cha tatizo lako. Una tatizo linalokusumbua? Unatafuta tiba bora? Kwa nini uendelee kutaabika?
Ofisi Zetu
Ofisi zetu ziko Dar es Salaam maeneo ya Upanga mtaa wa Lugalo,karibu kabisa na Palm beach hotel,mkabala na ubalozi wa Burundi.
Ni matumaini yangu kuwa hautajuta kuitembelea tovuti yetu, na kuchagua kutumia dawa zetu pia. Ni matumaini yangu kuwa utapata mahitaji yako katika tovuti hii nawe utapata msaada takiwa wakati wowote utakaouhitaji kwa ajili ya afya yako.
Wasiliana nasi wakati wowote kupitia barua pepe maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959 kwa ajili ya kupata msaada wowote utakaouhitaji. Pia toa maoni yako kuhusu mada yoyote uliyoisoma katika tovuti yetu. Ukiwa na swali,jisikie huru kabisa kuuliza nasi tutakujibu kwani ni furaha yetu kukuhudumia.
Karibu sana.


No comments
Post a Comment