Hepatitis A hueneaje?
-Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ya hepatitis A bila kusha mikono yake vizuri.
-Kunywa maji machafu
-Kula samaki wa baharini wasioiva
-Kugusana kwa karibu na mtu mwenya maambukizi
-Kujamiiana na mtu mwenye maambukizi hususani kama utagusa maeneo ya kutolea haja kubwa kwa vidole,mdomo au ulimi
-Kujidunga sindano aliyoitumia mtu mwenye maambukizi
Tiba Ya Hepatitis A
Inasemekana kuwa hakuna tiba kwa tatizo hili japo kwa muda fulani huweza kuisha lenyewe. Mtu aweza kufanya yafuatayo ili kupunguza madahra ya hepatitis A:
-Pata mapumziko ya kutosha
-Kunywa dawa za kupunguza maumivu
-Jiweke katika mazingira ya ubaridi,oga maji ya baridi,pata hewa ya kutosha,vaa nguo zinazouachia mwili na zisizobana ili kuepuka miwasho
-Kula chakula kidogo,rahisi kukusaidia kuepuka kichefuchefu na kutapika
-Usinywe pombe kuepuka kuendelea kudhuru ini
-Epuka kufanya tendo la ndoa tangia dalili za njano zilipojitokeza mwilini mwako
-Dumisha usafi kwa mfano osha mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara
-Mahusiano ya karibu kama vile kulala pamoja kama mume na mke,mnashauriwa kupata chanjo ya hepatiti A vaccine kuepuka kuambukizwa.
Unawezaje Kuzuia Maambukizi Ya Hepatitis A?
Kama tulivyoona hapo juu,unaweza kumwambukiza mwingine kama umeathiriwa na unaweza kuambukizwa kama huna virusi wanaosababisha ugonjwa huu. Mambo yafuatayo yatakuepusha kuambukizwa na kuambukiza wengine:
-Epuka kufanya mapenzi-Hepatitis A huweza kuambukiza zaidi katika wiki 2 za mwanzo tangu dalili zinapokuwa zimeonekana,epuka kufanya mapenzi katika kipindi hicho.
-Acha kuwaandalia wengine chakula kama utaweza
-Osha mikono yako kwa maji na sabuni kila mara utokapo chooni na kabla ya kuandaa chakula
-Usichangie taulo na vifaa vingine vya kuogea
-Safisha choo vizuri na mara nyingi kuliko wakati mwingine wowote
Tumeanza mada ya homa ya ini sehemu aina ya kwanza, hepatitis A. Katika mada itakayofuata tutaendelea kuangalia aina nyingine za hepatitis kama hepatitis B, C, D na E. Endelea kuwa nasi.
Usisahau kuweka maoni,ushauri au swali lako kuhusiana na mada hii.
Kama una tatizo la Hepatitis na unahitaji msaada,usisite kuwasiliana nasi kwa simu 0673 923 959 au tuandikie kwa barua pepe maishaniafya@gmail.com ili upate msaada unaotakiwa.



No comments
Post a Comment