Huenda mara baada ya kujifunza kuhusu chanzo na sababu za ugonjwa huu wa kisukari, ukawa unajiuliza utawezaje kuutambua. Na pengine huenda ukaanza kujiuliza kama kuna hatari yoyote ya kuwa na ugonjwa huu! Usiogope uko mahali sahihi, katika mada hii tutaangalia kwa kina sana dalili zake na madhara ya hatari zaidi yawezayo kutokana na kisukari.
Dalili za ugonjwa wa kisukari
Kwa namna fulani dalili hizi zimefichika. Na wakati fulani unaweza kudhani ni hali ya kawaida na unaweza usichukue hatua yoyote. Wengi wenye type 2 wamejikuta wakipata madhara makubwa ndipo wanashituka. Kwa type 1 dalili zake hutokea ndani ya muda mfupi na ni za haraka sana pengine katika siku kadhaa hivi au wiki kadhaa. Haya fuatana nami uone miongoni mwa haya ukiona linakupata ujue siyo hali ya kawaida bali na tatizo la sukari,
. Kukojoa mara kwa mara- Hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa sukari nyingi ndani ya mishipa ya damu, na maji mengi kutoka kwenye seli za mwili yatafyonzwa ili kuyeyusha sukari hii. kwa kadri linavyotokea hili figo italazimika kutoa sukari kwa njia ya mkojo na hivyo kujikuta ukikojoa mara kwa mara.
. Kupata kiu sana-kwa kadri maji yatakavyokuwa yakifyonza ili kuyeyusha sukari katika mishipa ya damu,maji yatapungua mwilini na kiu yako haitakauka.
. Kupatwa na njaa-kwa sababu hakuna insulin inayosaidia glucose kunyonywa na seli ili kutengeneza nishati mwili utakosa nguvu na kukutaka kula ili kurejesha nguvu inayopotea.
. Kupungua uzito-kwa kadri glucose inavyopotea ndivyo na mwili utakavyopoteza uzito wake.
. Uchovu wa mwili-mwili unapokosa nishati hupata uchovu.
. Ganzi mikononi na miguuni-sukari inapozidi mwilini husababisha kuharibiwa kwa mishipa midogo midogo ya damu inayoishia kwenye neva na kusababisha damu kutozunguka vyema na hivyo kusababisha ganzi.
. Kutoona vizuri-kuzidi kwa sukari huharibu lensi ya macho na kupelekea kushindwa kuona vizuri.
. Vidonda kushindwa kupona haraka-hii hutokana na kudhurika kwa neva za mwili.
. Kukauka kwa mdomo-kwa kuwa mwili unatumia maji mengi ili kutengeneza mkojo,maji yatapungu mwilini na mdomo kukauka.
. Ngozi kuwasha-hii nayoahutokana na madhara ya uwingi wa sukari mwilini.
. Kupoteza uwezo wa kufanya tendo la ndoa-mara nyingi hii huwakuta wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 wanapokumbwa na tatizo la sukari.
Madhara ya kisukari mwilini
Madhara ya kisukari ni makubwa sana ukilinganisha na uelewa wa walio wengi katika jamii. Nashawishika kufikiri kwamba kama tungeyatambua madhara yatokanayo na kisukari basi sisi
kama jamii tungejihadhari sana na ugonjwa wa kisukari kuliko kawaida.
-Magonjwa ya moyo; mgonjwa wa kisukari ana uwezekano wa zaidi ya mara 5 kuathiriwa na magonjwa ya moyo na kiharusi. Kutodhibitiwa kwa kiwango cha sukari mwilini huweza kusababisha magonjwa ya moyo kama Angina,Atherosclerosis n.k
-Kiharusi (Stroke); Sukari pia husababisha mirija ya damu kuziba kabisa na kusababisha kiharusi.
-Matatizo ya neva; kuzidi kwa sukari hupelekea kuharibika kwa neva. Neva za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula zikiharibiwa kwa mfano unaweza kuathiriwa na kichefuchefu,kutapika,kuhara na kiungulia mara kwa mara.
-Kupoteza uwezo wa kuona vizuri; mishipa ya damu kuelekea machoni inapokuwa na sukari nyingi kwa muda mrefu hupelekea kuharibika kwa retina tatizo linaloitwa Retinopathy na hivyo uwezo wa kuona hupotea.
-Matatizo ya figo; Katika figo kuna mishipa midogo sana inayochuja damu inayoingia kwenye figo na mishipa ya damu. Sukari nyingi huharibu mishipa hii inayoitwa nephron na kusababisha uharibifu wa figo tatizo linaloitwa Nephropathy.
-Kukosa uwezo wa kufanya tendo la ndoa; Kwa mwanaume hupatwa na matatizo ya jogoo kushindwa kuwika na hivyo uwezo wake kupotea kabisa lakini pia mwanamke hukosa hamu ya tendo,ukavu sehemu zake za siri n akupata maumivu makali wakati wa mchezo n.k
-Matatizo ya miguu; Kisukari hupunguza mtiririko wa damu katika miguu yako na kusababisha miguu kupoteza hisia kabisa na mara nyingine kupata ganzi. Unaweza kupata kidonda mguuni pasipo hata kuhisi kama umeumia na kidonda mguuni hushindwa kupona. Tatizo hili hupelekea wengine miguu yao kukatwa.
-Kuharibika kwa mimba ama kuzaa watoto walokufa; Wanawake wajawazito wenye ugonjwa wa kisukari (Gestational diabetes) huwa katika hatari kubwa ya kupata tatizo hili.
-Matatizo ya kusikia; sukari pia huweza kusababisha tatizo la kutosikia vyema.
-Ugumba; Kwa kuwa mtu mwenye kisukari hushindwa kufanya tendo la ndoa vyema aweza asipate mtoto pia.
Kufikia hapo ndugu msomaji natumaini umegundua na kuelewa vyema dalili na madhara ya ugonjwa huu wa kisukari. Mada ilopita tulitazama chanzo cha kisukari, nikualike katika mada itakayofuata upate kujua tiba na jinsi ya kudhibiti ugonjwa wa kisukari.
Je,unasumbuliwa na kisukari na unahitaji usaidiwe?
Inawezekana kabisa kuondokana na matatizo yote niliyoyataja hapo juu kwa kutumia bidhaa tulizo nazo. Kama unasumbuliwa na tatizo hili la kisukari tafadhali wasiliana nasi kupitia namba hapa chini.Kwa maoni,swali ama msaada tafadhali wasiliana nasi kupitia email address maishaniafya@gmail.com ama simu 0673 923 959.


No comments
Post a Comment