SABABU ZA MWANAMUME KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

Leo tutatazama tatizo lingine linalohusiana na ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume. Kwa kuwa neno upungufu wa nguvu za kiume ... thumbnail 1 summary










Leo tutatazama tatizo lingine linalohusiana na ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume. Kwa kuwa neno upungufu wa nguvu za kiume limekwishazoeleka mapema kutumika na watanzania walio wengi,niseme tunatazama aina nyingine ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hapa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume wengi hawapendi kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa,wakati hadi 46% ya wanawake huonesha kuridhika kuishi na tatizo hili.

Katika mada hii tutatazama nini husababisha mwanamume kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Ni kawaida kupoteza hamu ya tendo la ndoa kwa vipindi tofauti tofauti. Hamu ya tendo la ndoa hupungua pia kwa kadri umri unavyoongezeka japo siyo hivyo kwa wote,maana kuna wanaume wengi hufikia uzeeni huku wakiwa na uwezo na hamu ya kushirikiana na wenzi wao kimapenzi. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa ni tatizo kubwa kwa jamii kwa sasa,takribani mwanamume 1 kati ya 5 huwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa. Mara nyingi limekuwa likisababishwa na matatizo ya kisaikolojia na kimaisha pia. Fuatana nami sasa ndugu msomaji tunapoangalia sababu hizi na inawezekana ukapata msaada kupitia mada hii ikiwa una tatizo hili.




Chanzo cha  Mwanamume Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo la Ndoa Ni Nini?






Upungufu wa homoni ya Testesterone- Ni homoni ya kiume ambayo huimarisha misuli,huboresha uzito wa mifupa na huchochea utengenezwaji wa mbegu za kiume (sperms). Pia homoni hii  huongeza hamu ya tendo la ndoa. Kupungua kwa homoni hii inayozalishwa na korodani,husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa na uzalishaji wa mbegu za kiume huwa kwa kiwango kidogo.

Matumizi ya Dawa- Kutumia baadhi ya dawa huweza kupunguza uwezo wako wa kushiriki na mwenzi wako. Matumizi ya dawa kama za high blood pressure kama vile ACE na blocker huweza kusababisha uwezo wa kufanya mapenzi kupungua na hamu ya tendo la ndoa kupotea kabisa.

Mfadhaiko- Mfadhaiko huathiri utendaji kazi wa mwili wako wote. Mfadhaiko humfanya mtu apoteze kuvutiwa na kazi alizozoea kuzifanya hapo kabla ikiwa ni pamoja na tendo la ndoa. Imethibitika kuwa dawa za kupunguza mfadhaiko pia hupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mtumiaji.

Magonjwa ya muda mrefu- Kama unajisikia vibaya kutokana na ugonjwa wa muda mrefu,kufanya tendo la ndoa haitakuwa hitaji lako la kwanza. Magonjwa kama kansa hupunguza kiwango cha mbegu zako na hivyo hamu ya tendo la ndoa kupungua.







Kukosa usingizi-Imebainika kuwa tatizo la kukosa usingizi husababisha kupungua kwa kiwango cha homoni ya testesterone. Kupungua kwa homoni ya testesterone husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi pia.

Msongo wa mawazo- kwa mtu mwenye msongo uwezo wake wa kufanya tendo la ndoa hupungua. Hii ni kwa sababu msongo husababisha hitilafu kwenye mfumo wa homoni. Na hii huweza kupelekea mishipa ya ateri kubana na kuzuia damu kufikia sehemu muhimu zinazohusika na ufanyaji wa tendo la ndoa.

Kutojiamini- Haitawezekana kufanya tendo la ndoa kama wewe mwenyewe huamini. Kutojiamini hupelekea wasiwasi ambayo husababisha mvurugiko wa homoni zinazohusika kuongeza hamu na ufanyaji wa tendo la ndoa.

Pombe na Madawa ya kulevya- Matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha kupungua kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Matumizi ya madawa ya kulevya kama marijuana huharibu utendaji kazi wa tezi ya pituitari inayoratibu utengenezwaji wa homoni ya testesterone.

Jogoo kushindwa kuwika- Kukosa hamu ya tendo la ndoa ni matokeo ya jogoo kushindwa kuwika. Kama ulipatwa na tatizo la jogoo kushindwa kuwika husababisha wasiwasi na kutojiamini. Hii ni kwa sababu ya kufikiri kwamba huenda ikatokea tena. Hata hivyo jogoo kushindwa kuwika ni dalili ya uwepo wa tatizo kubwa la kiafya kama vile magonjwa ya moyo.

Unene uliopitiliza- Unene husababisha kupungua kwa homoni ya testesterone na kusababisha hamu ya tendo la ndoa kupungua. Pia unene huweza kusababisha magonjwa ya moyo na high blood pressure,ambayo kwa pamoja husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Mahusiano baina ya wenzi- Kama kuna magomvi,matukano na kupigana kati ya wenzi hamu ya kushiriki pamoja pia hupungua kama sio kutoweka kabisa. Lakini pia kama wenzi hawa wako mbali mbali pia hupelekea hamu ya kufanya mapenzi kupungua.

Umri mkubwa- Utengenezwaji wa homoni ya testesterone inayohusika na kuongeza hamu ya tendo la ndoa hupungua kwa kadri umri unavyoongezeka. Wanaume mara nyingi huanza kuhisi tatizo hili kuanzia miaka 60 hadi 65. Kupungua kwa homoni hii husababisha kupoteza hisia za tendo la ndoa na kuchelewa kufika kileleni.


Jinsi Ya Kutatua Tatizo La kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa 



Mambo ya kufanya ili kuongeza hamu ya tendo la ndoa yapo mengi. Hapa yapo machache tunayoweza kushauri ili ujue jinsi unavyotakiwa kufanya ili kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Mambo hayo ni kama yafuatayo;

Mazoezi- Kukosa hamu ya tendo la ndoa ni kwa sababu viungo fulani vimetulia pasipo kufanya kazi. Mazoezi huongeza ufanisi wa mzunguko wa damu,jambo linaloleta ufanisi wa tendo la ndoa. Kama umekuwa unafanya mazoezi,hebu ongeza tena kiasi fulani na kuongeza hamu na ufanisi katika ufanyaji wa tendo la ndoa.

Mridhishe mwenzi wako- Kukosa hamu ya tendo la ndoa pengine huwa ni matokeo ya tendo lililopita. Si mara zote tendo la ndoa hufanyika kwa ufanisi. Takribani 40% hadi 50% tu ya matendo ya ndoa huwa katika uthabiti na wenzi wote kufurahia. Kama mwanzoni hukumridhisha mwenzi wako, atatarajia awamu nyingine wewe kufanya vyema zaidi kuliko hapo mwanzo. Jitahidi kuondoa hofu na wasiwasi huku ukijiamini ili umridhishe mwenzi wako na ukidhi matamanio yake.

Jadilianeni Pamoja- Kujadiliana kwa pamoja hukusaidia kumfanyia mwenzi wako kile anachokitaka naue kukufanyia kile unachotaka. Hii itaongeza hamu yako kwa kuwa utapata unachotaka na mwenzi wako pia atapata anachotaka.








Jenga matamanio kwa mwenzi wako- Tendo la ndoa huazia akilini. Jenga mazoea ya kumwonw mwenzi wako kama bora sana na kitu atakachokufanyia ni bora sana pia. Unapopanga kushiriki na mwenzi wako,jenga picha akilini ya matamanio kwake na hii itakusaidia kuepuka kukosa hamu ya kushiriki na mwenzi wako.

Tumia chakula bora- Kuna uwezekano wa kutumia chakula ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Mchanganyiko wa chakula cha wanga kwa asilimia 40-50 ,protein kwa 25% -35%, fats kwa 25%-30% na matunda kwa wingi kama vile tikitimaji,husaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Pia virutubisho kama zinc na vig power huweza kukusaidia pia kuongeza uwezo na hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Epuka msongo wa mawazo- Kama tulivyoona hapo juu,msongo wa mawazo huweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, kuepuka msongo kutakusaidia kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi.

Mfumo wa maisha- Kama unataka kuepuka tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, epuka kutumia pombe kwa wingi. Epuka pia kutumia madawa ya kulevya kama vile marijuana na mengineyo.


Mpendwa msomaji,umeona jinsi tatizo hili lilivyo kubwa,na ilivyo muhimu kushughulika na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamume ili kuepusha hatari ya kumkoshesha mwenzi wako ama kuhatarisha mahusiano yako.Katika mada itakayofuata tutaliangazia tatizo la Jogoo Kushindwa Kuwika,sambamba na Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni.

Kama una tatizo hili na unapenda kuepukana nalo,usisite kuwasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie 0673 923 959,tutakusaidia.


Ni furaha yetu kupokea maoni,ushauri ama maswali kutoka kwako wewe msomaji wetu. Tafadhali usisite kutujulisha kupitia mawasiliano hapo juu.