Mfuko wa Nyongo ni kifuko kidogo kilicho chini ya kidogo ya ini. Mfuko huu mdogo wenye ukubwa kama wa pera hivi,hutunza nyongo inayotengenezwa na ini. Nyongo husaidia kumeng'enya chakula jamii ya mafuta (fats). Kabla ya kula chakula,mfuko wa nyongo huwa umejazwa na nyongo kabisa. Lakini baada ya kula chakula mfuko wa nyongo hubakia tupu,kwa sababu nyongo kusafirishwa kupitia mirija ya nyongo ili kusaidia umeng'enywaji wa chakula jamii ya mafuta (fats) katika utumbo mwembamba. Hapa tutakuwa tunatazama tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo aina ya ugonjwa wa nyongo.
Mawe kwenye mfuko wa nyongo sio mawe halisi,bali ni vipande vidogo vidogo vigumu katika mfuko wa nyongo. Si rahisi kujua kuwa una mawe haya ni hadi pale yatakapoziba mirija na kusababisha maumivu makali ambayo utatakiwa kuyatibu kwa haraka.
Aina za mawe kwenye mfuko wa nyongo:
Kuna aina mbili za mawe kwenye mfuko wa nyongo,aina hizi ni hizi;
.Cholestrol stones-hii hutokea pale kunapokuwa na kiwango kikubwa cha cholestrol kwenye mfuko wa nyongo. Haya ni mawe yenye rangi ya kijani-njano hivi. Ndiyo aina iliyozoeleka zaidi ambayo huathri zaidi ya 80% ya mawe ya mfuko wa nyongo yote.
.Pigment stones-haya ni mawe madogo madogo meusi. Hutokana na bilirubin ambayo hutengenezwa na nyongo. Wengi wanaopatwa na aina hii ni watu wenye matatizo ya ini,maambukizi ya mirija ya nyongo na sickle cell anemia.
Chanzo cha mawe kwenye mfuko wa nyongo-Gallstones
Kuna sababu tatu kubwa zinazosababisha hili tatizo la nyongo:
Kuzidi kwa cholestrol kwenye nyongo-kwa kawaida nyongo yako ina kemikali nyingi zinazoyeyusha mafuta (cholestrol) inayotolewa na ini lako. Pale ini litakapozalisha kiwango kikubwa cha cholestrol kuliko kile kinachoweza kuyeyushwa na nyongo,cholestrol hiyo hugandamana na kusababisha mawe.
Nyongo yako kuwa na Bilirubin nyingi-hii ni kemikali inayotengenezwa pale mwili wako unapovunja seli nyekundu za damu. Bilirubin hutengenezwa kwa wingi kunapokuwa na matatizo ya ini (liver cirrhosis),ugonjwa wa damu (sickle sell anemia). Uwepo wa bilirubin kuwa wingi husababisha mgonjwa kupatwa na huu ugonjwa wa nyongo.
Mfuko wa nyongo kushindwa kutoa nyongo yote-kama nyongo haitaisha wakati wote inapokuwa inatolewa ili kuingia kwenye utumbo mwembamba,nyongo hugandamana na kusababisha tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo.
Kwa hiyo ili kupata ugonjwa wa maumivu ya nyongo,sababu tajwa hapo juu zahusika. Zifuatazo hapa chini ni sababu zinazochangia moja wapo ya vyanzo tajwa hapo juu. Sababu hizi ni kama zifuatazo:
-uzito uliopitiliza
-Kupungua mwili wako (kukonda)
-Kuwa mjamzito
-Historia ya familia
-Kutumia vidonge vya uzazi wa mpango
-Kutokunywa maji kwa wingi
-kisukari
-Kutumia dawa za kupunguza cholestrol
-Kutumia dawa za kuongeza oestrogen
-Kuwa na ndugu wa karibu mwenye tatizo hili
-Mwanamke anayezaa zaidi ya miaka 40
-Upasuaji mkubwa
-Umri kuongezeka
-Kula vyakula vyenye fats nyingi
-Kutokula vyakula vyenye nyuzi nyuzi
-Kuwa na umri zaidi ya miaka 40
-Kuwa na tatizo la ini
Dalili za Mawe ndani ya mfuko wa nyongo (Gallstones)
Takribani 80% ya waathrika wa tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo huwa hawapati dalili kabisa,ni hadi pale daktari wako atakwambia. Lakini ukipata dalili zitakuwa ni kama zifuatavyo;
-Maumivu makali upande kulia juu ya tumbo
-Kucheua na miungurumo ndani ya tumbo baaada ya kula
-Kutapika mara kwa mara
-Maumivu makali upande wa bega la kulia
-Kutokwa jasho kwa wingi
-Maumivu makali ya mgongo katikati ya mabega
Madhara ya mawe ya nyongo (gallstones)
.Kuziba kwa mrija wa nyongo (cholangitis)-mawe kwenye nyongo yakizidi,huziba mirija inaopitisha nyongo kutoka kwenye mfuko wa nyongo au kwenye ini kwenda kwenye utumbo mwembamba.
.Maambukizi kwenye mfuko wa nyongo (cholesystitis)-hii hutokana na mirija ya nyongo kuziba kwa muda mrefu. Hii husababisha maumivu makali,homa na huhitaji upasuaji pale maambukizi yatakapozidi.
.Kuziba mrija wa kongosho (pancreatitis)-mrija huu huunganika na mrija wa nyongo. Juisi zinazotengenezwa kwenye kongosho ili kusaidia umeng'enywaji wa chakula kwenye utumbo mwembamba husafiri kupitia mrija wa kongosho (pancreatic duct). Mawe kwenye mfuko wa nyongo huziba mrija wa kongosho na kusababisha maambukizi ya bacteria kwenye kongosho hali inayosababisha maumivu makali na endelevu ya tumbo ambayo huhitaji tiba ya haraka.
.Kansa ya mfuko wa nyongo-mawe kwenye mfuko wa nyongo huweza kusababisha kansa ya mfuko wa nyongo. Japo hili huweza kutokea,si mara zote kansa hutokea. Ni watu wachache sana wanaopata kansa kutokana na tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo.
.Njano (jaundice)-mirija ya nyongo ikiziba na kuzuia nyongo kutoka kwa muda mrefu,sehemu nyeupe ya macho hubadilika na kuwa njano.
Jinsi ya kudhibiti tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo
-Kula chakula chenye afya-ukila mboga za majani,matunda na nafaka nzima utajiweka katika hatua nzuri ya kudhibiti tatizo la mawe ya nyongo kutokea.
-Jizoeze kunywa maji mengi kila siku hata kama huna kiu
-Dhibiti uzito wako katika kiwango kinachoendana na urefu wako. Tumia njia sahihi za kupunguza uzito wako,usiache kula eti upungue uzito,ukikonda pia unajiweka katika hatari zaidi ya kupata tatizo hili.
-Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi kwa wingi
Ndugu msomaji,tumetazama tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo. Kwa bahati nzuri tatizo hili sio hatarishi sana kiasi cha kumzuia mtu kuendelea na kazi zake. Wakati fulani tatizo likiwa kubwa hulazimu mfuko wa nyongo kuondolewa. Mfuko huu ukiondolewa mtu ataendelea kuishi pasina shida yoyote. Hii ni kwa sababu moja ya kazi za ini ni kuzalisha nyongo. Ini litaendelea kuzalisha nyongo na kuimwaga moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na maisha yataendelea kama kawaida bila mfuko wa nyongo.
Ndugu msomaji wangu leo tutaishia hapa katika mada hii. Mada itakayofuata tutaangalia
Chanzo Na Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo. Tafadhali endelea kuwa nasi katika mfululizo wa mada zetu zinazoendelea.
Kama una swali,maoni au ushauri wowote kuhusu mada hii tafadhali wasiliana nasi kwa njia yoyote ambayo ni rahisi kwako:maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959.
Una dalili au umegundulika kuwa na mawe kwenye mfuko wako wa nyongo? Tafadhali Wasiliana nasi upate msaada na tiba ya uhakika pasipo kemikali yoyote, muda wowote kwa simu 0673 923 959,au barua pepe maishaniafya@gmail.com


