Ugonjwa wa gout ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa maungio ya mifupa na kusababisha maumivu makali sana. Unasadikika kugundulika muda mrefu sana miaka ya 2640BC huko Misri na ukawa unaitwa ''ugonjwa wa kumfanya mtu asitembee''. Ni ugonjwa unatibika kabisa na wakati mwingine inawezekana kuudhibiti kwa kuchukua tahadhari kuuepuka kabisa. Katika mada hii tutaangalia gout ni nini? Chanzo cha gout ni nini? Tiba ya gout ni nini na Jinsi ya kuepuka ugonjwa wa gout.
Ugonjwa ni Gout ni ugonjwa gani?
Gout ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa joint. Ugonjwa huu huwapata sana wanaume kuanzia miaka 30-50 kuliko wanawake,japo wanawake wanapokoma hedhi huwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huu. Ugonjwa huu husababisha maumivu makali hasa katika joint za vidole,miguu hasa dole gumba,kiwiko ama goti. Kuvimba huku kwa joint husababishwa na kuzidi kwa tindi kali aina ya uric acid ambayo huzalishwa mwilini bila manufaa yoyote. Uric acid hujikusanya na kugandamana chini ya ngozi inayozunguka maungio ya mifupa.
Gout huweza kusababisha madhara ya kudumu katika maungio hayo ya mifupa au huweza kusababisha kidney stone (ugonjwa wa mawe ndani ya figo), kama mgonjwa hatapata matibabu kwa miaka 10 au zaidi.
Chanzo cha ugonjwa wa gout ni nini?
Kama nilivyosema hapo mwanzo gout ni moja ya magonjwa ya maungio ya mifupa - Arthritis unaotokana na kuzidi kwa uric acid mwilini. Hali hii hutokana na kuzalishwa kwa wingi kwa uric acid ama figo kuondoa uric acid kwa kiwango cha chini. Kwa kawaida uric acid huzalishwa ndani ya figo na kutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo. Uric acid hutokana na kuvunjwavunjwa kwa chakula aina ya purine (nyama,samaki wa baharini n.k) mwilini ndani ya figo. Chakula hiki kikivunjwa,uric acid hujikusanya,na hutakiwa kutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo,lakini hili lisipofanyika kwa ufasaha kiwango kikubwa cha uric acid hujikusanya kwenye maungio ya mifupa na hivyo kusababisha gout. Hali hii hasababisha kuvimba kwa sehemu hiyo na kusababisha maumivu makali na sehemu zilizo karibu. Mara nyingi kuzidi kwa uric acid huchangiwa na mazingira yafuatayo;
.Ulaji wa vyakula vyenye purine kwa wingi.
.Uzito kupita kiasi
.Kukaa au kuishi mazingira yenye madini ya lead.
.Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya ugonjwa huu.
.Matumiziya madawa ya jamii ya asprin na diuretic
. Kisukari
.Kuwana mafuta mengi kwenye mishipa ya damu
.Kuwa na matatizo ya moyo
.High blood pressure (Mgandandamizo mkubwa wa damu)
.Kunywa pombe kwa wingi
.Ajali ya mifupa hasa maeneo ya joint
. Kuwa na matatizo ya figo
. Kutumia madawa ya chemotherapy
Dalili za ugonjwa wa gout
Ugonjwa huanza kwa maumivu makali kwenye joint na mara nyingi huwa katikati ya usiku. Huambatana na maumivu makali kwenye joint na wakati mwingine hupelekea kuvimba kwa maungio ya mifupa na maumivu makali pia.
Tiba ya ugonjwa wa gout
Matatizo mengi ya gout huondolewa kwa kutumia dawa. Lakini katika mada hii ningependekeza matumiziya vyakula bora na mtindo mzuri wa maisha ili kuepuka na kuzuia tatizo la gout. Ni vyemaukafanya yafuatayo ili kuepuka ugonjwa wa gout na kupunguza tatizo pia;
-Kunywa maji mengi angalau lita 2 hadi 4 kwa siku.
-Kuwa na uzito sawia,epuka uzito ama unene kupindukia
-Pata mlo kamili
-Epuka matumizi ya pombe
-Epuka vyakula aina ya purine-vyakula vinavyozalisha uric acid kwa wingi. Mfano wa vyakula hivyo ni; Nyama (maini,moyo,figo), samaki wa baharini,uyoga nyama pori n.k
Hadi hapo tumeujadili sana ugonjwa wa gout moja kati ya magonjwa ya maungio ya mifupa-Arthritis. Ili kuyaelewa magonjwa mengine ya arthritis,usisite kusoma
magonjwa ya maungio ya mifupa -Arthritis na ili kujua magonjwa ya mifupa na umuhimu wa mifupa soma ukurasa wetu magonjwa ya mifupa. Usisite kutoa maoni yako ama kuuliza swali lolote kuhusiana na mada hii ikiwa lipo,kwetu ni furaha kukujibu kwa ufasaha.
Wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959. Pia usisite kutoa maoni yako ama ushauri kuhusu mada yetu ya leo.

