HOMA YA INI-HEPATITIS B

Ni ugonjwa wa homa ya ini amabo huenezwa kwa njia ya maji maji kama vile damu,maji maji ya ukeni au mbegu za kiume zenye maambukiz... thumbnail 1 summary








Ni ugonjwa wa homa ya ini amabo huenezwa kwa njia ya maji maji kama vile damu,maji maji ya ukeni au mbegu za kiume zenye maambukizi ya Hepatitis B virus (HBV). Kutumia vitu vya ncha kali kama vile nyembe au sindano na mtu aliye na virus au kujamiiana na mtu mwenye maambukizi  husababisha kusambaa kwa aina hii ya homa ya ini.



Chanzo Cha Hepatitis B




Chanzo cha homa ya ini (hepatitis b) ni virusi wa hepatitis b. Huweza kuenezwa kwa njia ya mwingiliano wa damu na maji maji ya mwilini kutoka kwa mtu aliyeathirika na virusi hawa. Virusi wanaosababisha maambukizi ya ugonjwa huu wa ini huzaliana na kuongezeka. Virusi hawa hawana uwezo wa kuduru ini moja kwa moja,badala yake uwepo wa virusi wanaosababisha maambukizi ya hepatitis b huamusha mfumo wa kinga ili kujaribu kuwadhibiti na kuzuia maambukizi zaidi. Utendaji kazi wa mfumo wa kinga kwa namna hii husababisha madhara kwenye ini na huweza kuharibu seli za ini kabisa.



Homa Ya Ini (Hepatitis B) Huenezwaje?







Aina hii ya homa ya ini huenezwa kwa njia ya mwingiliano wa damu na maji maji ya mwilini kutoka kwa mtu alipata maambukizi kwenda kwa mtu mwingine. Hili hutokea kupitia:

-Kufanya tendo la ndoa na mtu aliye na maambukizi bila kondomu

-Kuchangia sindano na mtu mwenye maambukizi

-Kuchorwa tatoo au kuchomwa na vitu vyenye ncha kali bila kuvifanyia usafi (sterization)

-Kuchangia nyembe au mswaki na mtu mwenye maambukizi

-Kuongezwa damu iliyo na maambukizi ya virusi wanaosababisha hepatitis b

-Kuchomwa kwa bahati mbaya na vitu vyenye ncha kali

-Damu kuingia kwa bahati mbaya sehemu iliyo wazi kama iwe kidonda au kung'atwa na mtu mwenye maambukizi ya virusi hawa.




Nani Anaweza Kupata Maambukizi Ya Hepatitis B




Watu walio kwenye hatari ya kupata maabukizi ya aina hii ya homa ya ini ni kama wafuatao:

-Watu wanaozaliwa maeneo yaliyo na maambukizi ya virusi hawa kwa wingi. Maeneo yenye maambukizi ya virusi hawa kwa wingi ni kama: nchi zilizo katika ukanda wa sahara,mashariki na kusini mashariki mwa bara la Asia,Visiwa cha Pasifiki,Baadhi ya sehemu za Amerika Kusini,Sehemu za kusini mwa Ulaya mashariki na kati,Mashariki ya kati na Sehemu za bara Hindi.

-Waatoto wanaozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Hepatitis B

-Watu wanaojidunga madawa

-Yeyote anayejihusisha na ngono isiyo salama

Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu hauenezwi kwa ya migusano ya kawaida kama kukumabtiana,kubusiana,kupiga chafya,kukohoa,kuchangia chakula na vinywaji au kushikana mikono.



Dalili Za Hepatitis B




Mtu huweza kupata maambukizi ya hepatitis B bila kujua kama ana tatizo. Si rahisi mtu kupata dalili za maambukizi ya virus wa hepatitis B. Na ikitokea ukapata dalili zitaweza kuonekana kuanzia miezi miwili hadi mitatu baada ya maambukizi ya virus. Dalili hizo zaweza kuwa:

-Kukosa hamu ya chakula

-Kuharisha

-Maumivu ya tumbo

-Homa ya manjano (jaundice)

-Uchovu

-Mwili kuuma

-Joto la mwili kuongezeka

-Mwili kuwa dhaifu

-Kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi






Madhara Ya Hepatitis B




Kama utapata matatizo ya homa ya ini isababishwayo na maambukizi ya virusi wa hepetitis b, ini lako huweza kudhurika vibaya. Hii huwapata wale waliopata maambukizi ya virusi hawa kwa muda mrefu bila kupata tiba. Miongoni mwa madhara ya maambukizi ya hepatitis B ni kama:


Liver Cirrhosis


Ni kudhurika (scarring) kwa ini kunakosababishwa na athari za muda mrefu kwenye ini. Tatizo hili huweza kuhusisha makovu au vidonda kwenye ini. Huweza kumwathiri mtu mmoja kati ya watano wenye maambukizi ya hepatitis b mara nyingi miaka mingi baada ya maambukizi.

Katika hatua za mwanzo si rahisi kujua kama ini limeathirika hadi pale utakapopata madhara zaidi. Athari za ini (cirrhosis) huweza kusababisha:

-Uchovu

-Kupoteza hamu ya kula

-Kupungua uzito

-Kujisikia dhaifu na mgonjwa

-Ngozi kuwasha

-Maumivu ya mwili

-Kuvimba kwa miguu na vifundo vya miguu



Kansa Ya Ini



Mtu 1 kati ya 20 wenye maambukizi ya hepatitis B kwa muda mrefu,huweza kupata kansa ya ini kila mwaka.

Dalili za kansa ya ini ni kama:

-Kupungua uzito kusiko kawaida

-Kupoteza hamu ya kula

-Kujisikia kushiba baada ya kul ahata kama chakula kilikuwa kidogo kabisa

-Kujisikia kuumwa

-Homa ya manjano (Jaundice)


Fulminant Hepatitis B



Hii ni hali inayotokea pale mfumo wa kinga za mwili kwa sababu ya uwepo wa virusi wanaosababisha hepatitis b,hushambulia seli za ini na kulidhuru ini vibaya. Tatizo hili hutokea kwa nadra angalau mtu 1 kati ya 100 mwenye maambukizi ya ini kwa muda mfupi (acute hepatitis B) huweza kupata tatizo hili.

Dalili zake huweza kuhusisha:

-Kuchanganyikiwa (confusion)

-Kuvimba kw atumbo kwa kuzidi maji

-Kupata homa kali ya manjano (severe jaundice)



Tiba Ya Homa Ya Ini - Hepatitis B





Tiba ya hepatitis b hutegemea muda gani umepita tangu ulipopata maambukizi. Kwa homa ya muda mfupi (acute hepatitis) na homa ya kudumu (chronic hepatitis).

Dawa ya Ini na Homa ya ini A,B,C,D na E
Bonyeza juu ya picha kusoma zaidi
Kwa homa ya ini ya muda mfupi mara nyingi huisha yenyewe bila tiba yoyote. Ukifanya mambo yafuatayo yaweza kukusaidia kuondoa dalili zako:

-Kupumzika

-Kula chakula chenye virutubisho

-Kunywa maji ya kutosha

-Epuka kunywa pombe

-Kutumia dawa na virutubisho vya asili

Homa ya ini ya kudumu huondolewa kwa kutumia dawa zinazoboresha na kuimarisha utendaji kazi wa ini. Kwa wengine hufanyiwa upasuaji w akubadili ini pale linapokuwa limedhurika sana.



Unawezaje Kudhibiti na Kuepuka Hepatitis B?




Chanjo ya heatitis B ni njia bor aya kudhibiti ugonjwa huu wa ini. Hii hutolewa kwa watoto,vijana na watu wazima wanapaswa kupewa chanjo. Kuepuka kupata au kusababisha maambukizi:

-Tumia kondomu wakati wa tendo la ndoa

-Usichangie sindano na mtu mwingine

-Vaa gloves unapogusa damu

-Usichangie nyembe na miswaki

-Epuka kuchorwa tatoo

Ndugu msomaji wangu tumekuwa sote katika mada hii ya Hepatitis B. Naamini ulifanikiwa kusoma mada iliyopita tulipoanza kuutazama Ugonjwa Wa Homa Ya Ini- Hepatitis,Mada itakayofuata tutatazama aina nyingine ya Homa Ya Ini-Hepatitis C. Karibu endelea kufuatana nasi.

Kwa maoni,maswali au ushauri usiache kutuandikia kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie simu 0673 923 959. Ni furaha yetu kukuhudumia.

No comments

Post a Comment