MAUMIVU KABLA YA HEDHI (PRE MENSTRUAL SYNDROME-PMS)

Karibu tena katika mwendelezo wa mada yetu hii tuliyoianza hapo mapema. Tumekwishaona jinsi hedhi inavyoweza kutokea katika mad... thumbnail 1 summary









Karibu tena katika mwendelezo wa mada yetu hii tuliyoianza hapo mapema. Tumekwishaona jinsi hedhi inavyoweza kutokea katika mada iliyotangulia. Katika mada hii tunaanza kutazama matatizo yanayoambatana na kutokea kwa hedhi. Matatizo hayo yaweza kuwa Premenstrual Syndrome (PMS), Premenstrual Dysphoric Disorder (PMDD) ama Dysmenorrhea. Katika mada hii tunaanza kutazama Premenstrual Syndrome. Karibu uendelee kufuatana nasi.

Premenstrual syndrome ni mfululizo wa mabadiliko ya kihisia,kitabia na kiafya kwa mwanamke ambayo huanza mara tu baada ya yai kutolewa (ovulation). Pia hufahamika kama Premenstrual Tension (PMT). Baada ya kitendo cha ovulation kunaweza kutokea mabadiliko mfululizo yanayoweza kuwa ya kihisia ama kitabia. Hili tunaweza kuliita tatizo,maana huathiri afya ya mwanamke kwa ujumla. Huambatana na maumivu makali kabla hadhi haijaanza na maumivu haya yaweza kupungua pale anapoanza kuingia mwezini. Takribani 85% ya wanawake wamekuwa wakipatwa na dalili za tatizo hili. Ni tatizo linaloweza kudumu kwa muda wa wiki moja hadi mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka (menstruation) na huisha pale tu hedhi (damu) inapoanza kutoka.


Chanzo cha Maumivu kabla ya Hedhi (Premenstrual Syndrome-PMS)


Chanzo cha maumivu kabla ya hedhi bado hakijajulikana. Kumekuwa na nadharia nyingi juu ya chanzo cha maumivu haya japo hakuna hata moja ambayo imethibitshwa kwamba husababisha maumivu kabla ya hedhi kutokea. Lakini watafiti wanasema huenda haya maumivu yakatokana na mabadiliko ya homoni za uzazi (sex hormones). Kiwango cha oestrogen na progesterone kikiwa juu sana kuliko kawaida,baadhi ya dalili za maumivu haya huweza kutokea. Lakini mambo yafuatayo huweza kuchangia sana kuongeza maumivu lakini hayasababishi maumivu haya kutokea;

.Kuwa na mfadhaiko
.Kuwa na mahusiano ya kifamilia na waliowahi kupata tatizo hili
.Kuwa na mahusiano ya kifamilia na wanafamilia wenye mfadhaiko
.Kula chumvi kwa wingi kwenye vyakula
.Kunywa pombe
.Kutumia caffeine kwa wingi
.Kukosa usingizi wa kutosha



Dalili za Maumivu kabla ya Hedhi (Premenstrual syndrome-PMS)



Premenstrual syndrome (Maumivu kabla ya hedhi) hujionesha katika dalili kadha wa kadhalakini si akin mama wote wataweza kupatwa na dalili hizi.Wengine huonekana kupatwa na dalili nyingi na wengine huoekana kupatwa na dalili chache sana katika hizi tunazokwenda kuzitazama sasa.
Dalili hizi zimegawanyika kimaumbile,kihisia na kitabia. Hebu tuziangalie sasa ili hapo utakapoona moja kati ya hizo ujue ni tatizo hili linakukabili.


Dalili za Kimaumbile

-Maumivu makali
-Matiti kuuma yakiguswa
-Kichwa kuuma
-Kupata njaa kali na kupenda kula sana
-Misuli kuuma
-Maungio ya mifupa (joint) kuuma
-Kuvimba mikono na miguu
-Kupata chunusi
-Kuongezeka uzito
-Kuharisha

Dalili za kihisia

-Kuwa na wasiwasi
-Mfadhaiko
-Kulialia
-Kukosa usingizi
-Kupenda kukaa peke yako na kujitenga na jamii
-Kuwa na hasira


Dalili za kitabia

-Kuchoka
-Kusahausahau
-Kukosa tafakari njema ya akili



Tiba ya maumivu kabla ya hedhi (premenstrual syndrome-PMS)


Tiba ya premenstrual syndrome bado ni changamoto kama ambavyo chanzo pia bado ni changamoto. Kinachofanyika sasa ni kupunguza maumivu haya ili mwanamke huyu apate ahueni. Kuna dawa hutolewa hospitalini kwa ajili ya kupunguza maumivu kama vile Diuretics,pain killers,Benzodiazepines,ovarian suppressors,antidepressants na nyinginezo.

Virutubisho kama vile calcium,magmesium,vitamin D na vitamin E vimethibitika kupunguza maumivu kabla ya hedhi kabisa na mwanamke mwenye maumivu kuondokan ana maumivu haya.











Lakini pia kuna mambo ambayo mwanamke mwenye tatizo hili akiyafanya aweza kudhibiti maumivu
ya kabla ya hedhi na kuendelea vizuri kabisa. Mambo hayo ni kama yafuatayo;

-Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku
-Pata chula bora chenye virutubisho kama vile nafaka nzima (isiyokobolewa),matunda na mboga za majani
-Tumia calcium kwa wingi
-Epuka kutumia chumvi nyingi kwenye chakula
-Epuka matumizi ya caffeine
-Acha kuvuta sigara
-Acha kunywa pombe
-Pata usingizi wa kutosha
-Ondokana na mazingira na yote yanayokuletea msongo na fadhaa.


Tumefanikiwa kulitazama kwa undani tatizo la maumivu kabla ya hedhi,na mapendekezo ya tiba ili kuondokana nalo ama kuliepuka katika mada hii. Ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili na unatafuta tiba tafadhali usisite kuwasiliana nasi ili uweke afya yako katika hali nzuri maana tunalimudu kabisa kupitia bidhaa zetu tulizo nazo.

Katika mada itakayofuata tutatazama maumivu wakati wa hedhi. Katika uhalisia kuna wanawake wengi wanaosumbuliwa na tatizo hili,kwamba kila hedhi yake inapoanza,moja kwa moja yeye pia hupata maumivu makali ya tumbo hadi pale inapoisha.


Kama umekuwa mhanga wa tatizo hili usisite kuwasiliana nasi ili upate msaada wa karibu na haraka.Wasiliana nasi kupitia Simu 0673 923 959 ama tuandikie kupitia maishaniafya@gmail.com.

 Ikiwa una maoni ama swali kuhusiana na mada hii,tafadhali usisite kutuandikia ama kutujilisha kwa njia yoyote iliyo rahisi kwako maana tunapenda sana kusikia toka kwako.



Karibu,