Kwa sasa tatizo la unene uliopindukia ni mara mbili ya hali ilivyokuwa miaka ya 1980. Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO),kufikia mwaka 2014,takribani watu bilioni 1.9 wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea duniani walikuwa na tatizo la uzito uliopitiliza kati yao watu milioni 600 walikuwa na tatizo la unene uliopitiliza. Watoto milioni 41 wenye umri wa miaka mitano na kuendelea walikuwa na tatizo la uzito uliopitiliza na wanene. Kwa kawaida unene na uzito uliopitiliza ni matatizo yanayoua watu wengi sana kuliko unene na uzito pungufu.
Madhara Ya Unene Kupita Kiasi Ni Yapi?
Athari za unene uliopindukia ni kusababisha matatizo mengi ya kiafya. Kwa mtu mwenye tatizo la unene uliopitiliza huwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa hatarishi kama hataweza kudhibiti tatizo kwa haraka. Madhara ya unene kupita kiasi huweza kuwa ni yale yanayoonekana siku kwa siku au kupata magonjwa hatarishi.
Matatizo ya siku kwa siku ya unene kupita kiasi:
-Kupumua kwa shida-Kutokwa jasho kwingi
-Kukoroma ukiwa umelala
-Kushindwa kufanya shughuli za nguvu
-Kujisikia mchovu mara kwa mara
-Maumivu ya joint na mgongo
-Kushindwa kujiamini na kutojikubali
-Kujihisi umetengwa
-Huweza pia kusababisha mfadhaiko
Magonjwahatarishi yanayoweza kusababishwa na kuwa na unene uliopitiliza ni kama yafuatayo:
-Kisukari aina ya 2
-High blood pressure
-High cholestrol (lehemu nyingi)
-Asthma
-Kiharusi (Stroke)
-Ugonjwa wa mishipa ya moyo (Coronary heart disease)
-Aina tofauti za kansa kama vile kansa ya utumbo mpana,kansa ya matiti na kansa ya mfuko wa mimba
-Mawe kwenye mfuko wa nyongo (gallstone)
-Ugonjwa wa maungio ya mifupa wa Osteoarthiritis
-Magonjwa ya ini
-Magonjwa ya figo
-Kisukari wakati wa ujauzito (gestational diabetes)
-Presha ya mwanamke wakati wa ujauzito (Pre-eclampsia)
Unene uliopitiliza huweza kupunguza urefu miaka ya kuishi kwa takribani miaka 3 hadi 10 kulingana na kiwango tatizo lilichofikia. Kwa Ulaya unene kupindukia unakadiriwa kusababisha kifo cha mtu 1 kati ya watu 13.
Suala la kupunguza uzito wa mwili sio mchezo. Linahitaji kujitolea na maamuzi thabiti na hufanya kazi vyema kama utakamilisha dozi au ratiba yote. Katika mada itakayofuata tutajadili jinsi ya kupunguza uzito au unene uliopitiliza.
Kama una swali,maoni au ushauri kuhusiana na mada hii,tafadhali usisite kutuandikia kupitia maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959.


No comments
Post a Comment