Maumivu wakati wa hedhi kitalaamu ni tatizo linalojulikana kama Dysmenorrhea au Menstrua Cramp. Takribani nusu ya wanawake wote hupata maumivu wakati wa hedhi,na takribani 15% hupata maumivu makali sana wakati wa hedhi. Wengi wanaopatwa na maumivu makali ni wale wenye msongo mkubwa wa mawazo,mabinti chini ya miaka 20,wanaopevuka wakiwa wa maika 11,wanaotokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi na wale ambao hawajazaa kabisa.
Katika mada hii tutaangalia kwa nini maumivu hutokea,dalili na tiba yake.Kwa kuanza hebu kwanza tuangalie aina.
Kuna aina mbili za maumivu wakati wa hedhi;
Primary Dysmenorrhea-Ni maumivu ya hedhi ambayo huja na kutoweka kila mwezi bila kusababishwa na ugonjwa wowote. Maumivu haya pengine huanza siku 1 au 2 kabla au pale tu anapoingia kwenye siku zake,na huhisiwa zaidi chini ya kitovu,chini ya mgongo na kiunoni. Haya ndiyo maumivu yayowathiri wanawake wengi sana hasa wenye umri mdogo,zaidi ya 50% na 15% kati ya hao hupata maumivu makali sana. Mwanamke huweza kupata maumivu haya kwa siku 2 hadi 4 yakiambatana na kichefuchefu,kutapika,uchovu na pengine kuharisha. Maumivu hupungua kwa kadri mwanamke anavyokuwa mkubwa (kiumri) na hupungua zaidi mwanamke anapopata mtoto.
Secondary Dysmenorrhea- Ni maumivu ambayo husababishwa na magonjwa katika viungo vya uzazi wa mwanamke. Magonjwa haya yakitibika humfanya mwanamke huyu kuondokana na maumivu haya. Magonjwa haya ni kama Endometriosis,adenomysis,fibroids au maambukizi ya wadudu. Haya huanza na kuisha kwa muda mrefu kuliko kawaida na hayaambatani na dalili zozote kama kutapika,kichefuchefu ama kuharisha.
Chanzo cha maumivu ya Hedhi (Menstrual Cramps)
Maumivu haya kama tulivyoona hapo juu,yamegawanyika katika aina mbili,na sababu za kutokea kwake nazo zinatofautiana. Tuanze na primary Dysmenorrhea.
Primary dysmenorrhea pia huitwa common menstrual cramp (maumivu ya kawaida). Chanzo cha maumivu haya ni ya kawaida kwa sababu hutokea kwa sababu ya mzunguko wa hedhi. Katika wakati wote wa hedhi kuta za uterus hukakamaa na kukaza kwa sababu ya uwepo wa kemikali ya postglandin. Hedhi inapoanza kutoka,kuta hizi hukakamaa na kukaza zaidi na zaidi. Mfuko wa mimba (uterus) unapokaza zaidi,huiminya mishipa ya damu inayozunguka mfuko wa mimba na kuzuia oxygen kuifikia. Mishipa ya damu ya uterus inapokosa oxygen ya kutosha maumivu hutokea.
Kwa upande wa secondary dysmenorrhea,yafuatayo yaweza kusababisha;
.Endometriosis-Ni hali ambapo tishu zinazojenga kuta za ndani za uterus,hujenga nje badala ya ndani.
.Adenomyosis-Ni hali ambapo tishu zinazojenga kuta za uterus huanza kujijenga kwenye misuli ya uterus.
.Pelvic Inflammatory Disease-Ni maambukizi ya bacteria yanayoanzia kwenye uterus na kuenea kwenye viungo vingine vya uzazi.
.Cervical stenosis- Ni kupungua kwa upenyo wa cervix na hivyo kuzuia hedhi kutoka.
.Fibroids-Ni uvimbe usio wa kansa ndani ya mfuko wa uzazi.
Dalili za maumivu wakati wa Hedhi
Dalili kubwa ni maumivu makali chini ya kitovu na kwenye nyonga. Pengine huweza kuwa mgongo na kiuno pia. Lakini pamoja na hayo dalili nyingine zaweza kumpata mwanamke pia kama zifuatazo;
-Maumivu makali chini ya tumbo,chini ya mgongo na mapaja-Kichefuchefu
-Kutapika
-Kichwa kuuma
-Kutokwa jasho sana
-Kizunguzungu
-Kukosa choo
-Kichwa kuwa kizito sana na kuzimia
-Uchovu
Jinsi ya kuondoa Maumivu ya Hedhi
Mambo yafuatayo waweza kuyafanya ili kuondokana na maumivu wakati wa hedhi;
1. Fanya mazoezi
Wanawake wanaofanya mazoezi,hupata maumivu kidogo kuliko wasiofanya mazoezi. Ili kupunguza maumivu yako,jitahidi kuweka mazoezi kwenye ratiba zako za kila siku.
2.Chakula
Tafiti zimeonesha kuwa matumizi ya fatty acid (omega-3),vitamin E,thiamine,vitamin B6 na Calcium huweza kuondoa maumivu wakati wa hedhi.
3.Joto
Pata joto kwa kujiweka ndani ya bafu la maji yenye joto kama inawezekana. Ila waweza pia kutumia kitambaa kilicholowekwa ndani ya maji ya moto na kukiweka chini ya kitovu.
4.Ondoa Msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo huongeza maumivu yako kwa kiwango kikubwa,na kuptokuwa na mawazo hupunguza maumivu yako.
5.Acha kutumia pombe na tumbaku
Kuepuka pombe na tumbaku kutakusaidia kupunguza maumivu yako maana huongeza maumivu kwa kiwango kikubwa.
6.Epuka matumizi ya caffeine
Hii pia ni kama mafuta yanayochochea maumivu.
7.Pata mapumziko inapobidi
Maumivu wakati wa hedhi yana tiba na hivyo kama unakabiliwa na tatizo hili. Kuna dawa za kupunguza maumivu,na upasuaji kwa mtu mwenye chanzo bainishi kama tulivoona hapo juu kwenye secondary dysmenorrhea. Kama una maoni ama swali kuhusa mada hii waweza wasiliana nasi pia. Lakini ikiwa hili limekuwa tatizo lako kwa muda mrefu,usiwaze suluhisho lake lipo.
Maumivu wakati wa hedhi ni matokeo ya mzunguko wa hedhi kwa mwanamke kila mwezi. Mada iliyopita tulikuwa na mada ya maumivu kabla ya Hedhi-Premenstrual Syndrome (PMS). Katika mada itakayofuata ndugu msomaji tutazungumza juu ya Mwanamke kukosa Hamu ya tendo la Ndoa. Endelea kufuatana nasi.
Je,unapata maumivu makali kwenye hedhi yako? Kama unahitaji msaada,Wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au simu 0673 923 959.
Usisite kutoa maoni yako kuhusiana na mada hii.

