LIJUE TATIZO LA BAWASIRI-PILES

Inawezekana umekuwa na tatizo katika sehemu yako ya kutolea haja kubwa. Labda unajisikia maumivu au panatoka damu na pengine unawe... thumbnail 1 summary








Inawezekana umekuwa na tatizo katika sehemu yako ya kutolea haja kubwa. Labda unajisikia maumivu au panatoka damu na pengine unaweza kuona vijinyama vinatokeza sehemu hiyo. Hili ni tatizo la bawasiri. Katika mada hii tutalitazama tatizo la bawasiri. Je bawasiri ni kitu gani,chanza,dalili na tiba yake ni ipi? Haya yote tutayatazama katika mada hii.


Bawasiri Ni Nini?


Bawasiri (Piles) hutokana na kuvimba kwa vena zinazopatikana sehemu ya kutolea haja kubwa. Kila mtu ana vena (haemorrhoids) hizi na hazina madhara yoyote mwilini. Ni pale vena hizi zinapovimba na kuwa kubwa kuliko kawaida ndipo tatizo linapotokea. Hivyo Bawasiri (piles) ni uvimbe wa vena zinazopatikana ndani au kuzunguka tundu la kutolea haja kubwa.

Uvimbe huu huweza kutokea ndani ya tundu la kutolea haja sentimita 2 hadi 4 kutokea nje ya tundu la kutolea haja kubwa au huweza kutokea nje kuzunguka sehemu ya kutolea haja kubwa.


Aina za Bawasiri


Kuna aina mbili za Bawasiri:

i. Bawasiri za ndani (Internal Haemorrhoids)-ni bawasiri zinazotoka ndani sentimita 2 hadi 3 kutokea sehemu ya juu ya kutolea haja kubwa. Hii ndiyo aina ya bawasiri iliyozoeleka sana. Aina hii ya bawasiri huweza kugawanywa katika madaraja manne (4).

.Daraja la 1-ni uvimbe mdogo usionekana ndani ya tundu la kutolea haja kubwa

.Daraja la 2-ni bawasiri kubwa kidogo kuliko za daraja la 1. Nazo huwa ndani ya tundu la kutolea haja kubwa na wakati wa kujisaidia huweza kutoka nje lakini kurudi ndani zenyewe.

.Daraja la 3-ni bawasiri ambazo huning'inia nje na wakati fulani mhanga huzirudisha ndani kwa vidole.

.Daraja la 4-ni bawasiri kubwa kabisa ambazo huning'inia nje ya tundu la kutolea haja kubwa muda wote. Bawasiri hizi haziwezi kurudishwa ndani ya tundu kama za daraja la 3 na hizi huhitaji tiba ya haraka.




ii. Bawasiri Za Nje (External Haemorrhoids)-ni bawasiri ambazo hutokea juu ya tundu la kutolea haja kubwa. Hizi huwasha sana na kuwa na maumivu kama damu itaganda ndani yake.



Chanzo Cha Bawasiri




Chanzo rasmi cha bawasiri bado hakijulikani japo huhusishwa kwa karibu na uwepo wa msukumo mkubwa wa damu kwenye mishipa ya damu ndani na kuzunguka sehemu ya haja kubwa. Msukumo wa huweza kusababisha mishipa ya damu maeneo ya haja kubwa kuvimba na kudhurika. Miongoni mwa sababu kubwa za kutokea kwa tatizo hili ni:

-Kukosa choo kwa sababu ya kukosa vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa wingi. Hili husababisha kujikamua kwa nguvu sana unapokuwa unajisaidia na pia husababisha kukaa muda mrefu chooni,jambo ambalo pia ni hatari.






-Tatizo endelevu la kuharisha hudhoofisha tishu na misuli inayozunguka au iliyo karibu na tundu la kutolea haja kubwa.

-Unene au uzito kupita kiasi

-Umri kuongezeka kwa sababu tishu zinazozunguka sehemu ya kutolea haja kubwa hudhoofika

-Kuwa mjamzito ni kawaida kupata bawasiri kwa sababu msukumo wa damu huongezeka kwenye mishipa chini ya nyonga kwa sababu ya mtoto kubana.

-Kuinua vitu vizito mara kwa mara

-Kuwa na wanafamilia wenye tatizo hili kwa sababu imeonekana kwamba ni tatizo linaloweza kurithiwa.

-Kuwa na kikohozi endelevu na kutapika mara kwa mara

-Kukaa kwa muda mrefu



Dalili Za Tatizo La Bawasiri








Mara nyingi bawasiri haisababishi dalili zozote na watu wengi hushindwa kujua kama wana tatizo hadi pale wanapokuwa wameathirika kabisa. Lakini kama dalili zikitokea huweza kuwa:

-Kutokwa na damu baada ya kujisaidia haja kubwa

-Kuwashwa maeneo ya haja kubwa

-Kutokwa na ute ute baada ya kujisaidia

-Kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa baad aya kujisaidia

-Maumivu wakati wa kujisaidia

-Sehemu inayozunguka eneo la haja kubwa kuwa nyekundu na vidonda

Bawasiri huwa haina dalili za maumivu labda kama kuna upungufu wa damu kwenye mishipa ya damu karibu na eneo la kutolea haja kubwa.




Tiba Na Jinsi Ya Kudhibiti Bawasiri




Mambo yafuatayo yanaweza kusaidia kuepuka,kudhibiti na kuondoa tatizo la bawasiri:

-Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa wingi kama vile nafaka nzima,matunda na mboga za majani. Pia kunywa maji kwa wingi yatasaidia kulainisha choo.

-Epuka kutumia caffeine si nzuri

-Punguza unene au uzito uliopitiliza,kama uzito wako ni mkubwa kupita kiasi basi jitahidi kuupunguza.

-Fanya mazoezi mara kwa mara,mazoezi husaidia kulainisha choo na kupunguza msukumo wa damu kwenye mishipa ya haemorrhoids (veins zilizo kwenye eneo la kutolea haja).

-Epuka kujikamua sana unapoenda chooni kwa sababu itaongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu inayozunguka sehemu ya kutolea haja

-Tumia nyuzi nyuzi za nyongeza ili kuepuka tatizo la kukosa choo.

-Fanya zoezi la kuketi kwa muda angalau dakika 15 hadi 20 hivi inchi kadhaa juu kutoka kwenye maji ya uvunguvugu kutasaidia kupunguza uvimbe wa bawasiri.

-Epuka kukaa kwa muda mrefu

-Kausha kabisa sehemu ya haja kubwa vyema kila mara unapopafanyia usafi. Fanya usafi mara kwa mara kuepuka kutokea kw atatizo la bawasiri

-Jisaidie kila inapotakiwa ili kuimarisha afya ya misuli na mishipa ya damu inayozunguka na ndani ya tundu la kutolea haja kubwa.

Tumetazama kwa undani tatizo la bawasiri. Tumetazama aina zake,chanzo,dalili n atiba za bawasiri. Naamini umepata msaada sahihi na unaokidhi kulifahamu kwa kina tatizo la bawasiri. Kama una sawi,maoni au ushauri kuhusiana na mada hii tafadhali usisite.

Kwa bahati nzuri bawasiri ni tatizo linalotibika kabisa. Kama una tatizo la bawasiri na hujui upate tiba wapi,tafadhali wasiliana nasi kupata tiba bora kwa ajili ya afya yako. Piga simu 0673 923 959 au tuandikie kupitia maishaniafya@gmail.com.






No comments

Post a Comment