Karibu leo tena ndugu msomaji wangu katika mada ya siku ya leo. Leo tutatazama tatizo la homa ya ini,ni kitu gani,hutokeaje,madhara na tiba yake ni ipi, yote tutayaangalia katika mada hii.
Ini ni kiungo kikubwa kuliko vingine ndani ya mwili wa biandamu. Ini hupatikana upande wa kulia juu kidogo ya tumbo na figo la kulia ndani ya kiwambo cha kifua (diaphram) . Damu huingia ndani ya ini kutoka kwenye Aorta kupitia mshipa wa hepatic artery na huchukuliwa kuelekea kwenye mshipa wa vena cava kupitia hepatic veins. Lakini pia mshipa wa hepatic portal vein huleta damu yenye virutubisho toka kwenye utumbo mwembamba ndani ya ini. Ini hufanya kazi nyingi sana mwilini huenda kuliko kiungo kingine chochote. Hebu tutazame kwa ufupi baadhi ya kazi za ini.
Kazi Za Ini
Kama tulivyoona hapo juu,ini hufanya akzi nyingi sana kuliko kiungo kingine chochote mwilini. Hebu tuangalie baadhi ya kazi za ini:
-Kutengeneza nyongo ambayo husaidia kumeng'enya chakula aina ya mafuta ndani ya utumbo mwembamba
-Kutengeneza proteins
-Kutengeneza mafuta (cholestrol) na aina fulani ya protein zinazosaidia kusafirisha mafuta mwilini
-Kuhifadhi na kutoa sukari (glucose) kila inapohitajika
-Kuchakata haemoglobin ili madini ya chuma yaliyo ndani yake yatumike
-Kubadili ammonia kwa kuwa huwa na madhara na kuwa urea ambayo hutolewa kwa njia ya mkojo
-Kuondoa sumu na madhara yatokanayo na madawa na vitu vingine vyenye madhara
-Kudhibiti kuganda kwa damu
-Kuzuia maambukizi kwa kuzalisha kinga na kuondoa bacteria kwenye damu
-Kuondoa bilirubin-uchafu utokanao na kuvunjwa kwa chembe chembe hai nyekundu za damu. Kama bilirubin itazidi mwilini utapata njano (jundice)
-Kuhifadhi vitamini A,D,K na B12 na madini ya chuma
-Kubadili suakri iliyotunzwa kama glycogen ili kutengeneza glucose itumike mwilini
-Huvunjavunja haemoglobin,insulini na homoni nyinginezo
Homa Ya Ini (Hepatitis)
Hepatitis kwa ufupi ni maambukizi kwenye ini. Mara nyingi husababishwa na virusi japo wakati mwingine huweza kuwa na sababu nyingine. Sababu nyingine huweza kuwa shambulio la kinga za mwili kwenye ini (Autoimmune hepatitis),madawa,sumu na pombe.Kuna nyingi za hom aya ini (Hepatitis A,B,C,D,E na kadhalika). Japo kuna aina nyingi za hepatitis,dalili zake ni zile zile.
Dalili Za Homa Ya Ini (Hepatitis)
Watu wengi hupata dalili kidogo sana au pengine hukosa dalili kabisa wanapokuwa na tatizo la homa ya ini. Lakini kama dalili zitatokea zitaonekena kuanzia siku ya 15 hadi 180 baada ya maambukizi. Dalili za ugonjwa wa homa ya ini hufanana kwa aina zote za homa ya ini. Kama dalili zitanekana katika hatua za mwanzo (Acute hepatitis) zitaweza kuwa:
-Kuharisha
-Uchovu
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupata homa kwa mbali
-Maumivu Ya Misuli Na Maungio Ya Mifupa (joints)
-Kichefuchefu
-Maumivu ya tumbo kwa mbali
-Kutapika
-Kupungua uzito
-Kupata njano (Jaundice)
Mara nyingi dalili hizi katika hatua za awali (acute hepatitis) huwa hazina madhara makubwa lakini kwa baaadhi ya watu huweza kusababisha ini kushindwa (Liver failure) au kifo. Lakini pia huweza kusababisha maambukizi endelevu (chronic infections). Mara nyingi hii hutokea kwa hepatitis B na C. Kwa kadri ugonjwa utakavyoondelea,utaweza kusababisha kushindwa kwa ini kuliko endelevu (progressive liver failure) huweza kusababisha njano,kuvimba miguu na vifundo vya miguu,kuchanganyikiwa (confusion),kutapika na damu kwenye kinyesi. Kama hatua hii itafikiwa haya yaweza kutokea:
-Mkojo mweusi
-Mkanda wa jeshi (hives)
-Ngozi kuwasha
-Kujisaidia kinyesi chenye rangi ya mwanga
-Ngozi na macho kuwa ya njano
Aina Za Homa Ya Ini (Hepatitis). Ziko aina tano kama tutakavyoangalia hapa yaani hepatitis a,b ,c ,d na e. Karibu uwe nasi.



No comments
Post a Comment