KUWAHI KUFIKA KILELENI-PREMATURE ENJACULATION (PE)

Kuwahi kufika kileleni ni tatizo lingine la nguvu za kiume linalosumbua wanaume wengi katika jamii yetu leo. Ni pale mwanaume... thumbnail 1 summary











Kuwahi kufika kileleni ni tatizo lingine la nguvu za kiume linalosumbua wanaume wengi katika jamii yetu leo. Ni pale mwanaume anapofikia kilele cha tendo la ndoa kabla ya mwenzi wake. Inakadirirwa katika wanaume 3 kuna 1 mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni. Mtu husemwa kuwa ni mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni kama mara zote atamaliza ndani ya sekunde 30 hadi dakika 1 hivi baada ya kuanza tendo la ndoa au hata kabla ya hajaanza. Utafiti uliofanyika kwa zaidi ya wanandoa 500 ulibaini kuwa muda uliochukuliwa kufika kileleni ilikuwa ni kama dakika 5 hivi. Kwa upande mwingine hakuna muda rasmi wa wenzi kufika kileleni,kwa sababu hili hutegemea maamuzi ya wenzi peke yao.

Ikiwa unafika kileleni au kumwaga mapema hata kabla hujaingia mara kwa mara,au kama huwezi kabisa kujizuia na kitendo cha kufika kileleni muda wowote mara nyingi, au kama una uoga hadi kuhofia kufanya tendo la ndoa kwa kuogopa kumaliza mapema pindi utakapokutana na mwenzi wako, basi wewe utakuwa na tatizo hili la kuwahi kufika kileleni haraka. Wanaume walio wengi huogopa ama kuona aibu kuweka wazi kama wana tatizo la nguvu za kiume,lakini nje ya aibu tatizo la kuwahi kumaliza linalotibika kabisa.

Katika mada hii tutatazama baadhi ya mambo yanayochangia mwanaume kufika kileleni mapema,na jinsi anavyoweza kufanya kuliepuka ama kulitibu kabisa tatizo hili.




Chanzo cha kuwahi kufika kileleni




Chanzo cha tatizo hili bado hakijafahamika bado. Mwanzoni ilidhaniwa kuwa chanzo ni sababu za kisaikolojia tu lakini watalaamu wa afya sasa wamegundua kuwa kuwahi kufika kileleni huchangiwa pia na sababu za kibailojia. Kwa kuanza hebu sasa tuanze kutazama sababu za kuwahi kufika kileleni kwa wanaume.


Sababu za Kisaikolojia

-Uzoefu wa mapenzi uliopita
-Migogoro ya kimahusiano
-Msongo wa mawazo
-Kuhisi raha zaidi
-Kuhisi hatia au kutojiamini
-Mfadhaiko
-Mwonekano wa mwili
-Hofu ya kumaliza haraka


Sababu za kibailojia



-Maambukizi kwenye tezi ya prostate au kwenye mrija wa urethra
-Kiwango kidogo au kikubwa cha homoni hususani thyroid
-Kisukari
-Kiwango kidogo cha visafirisha taarifa (neurotransmiter) kwenye ubongo
-Madawa ya kulevya
-Kunywa pombe nyingi
-Tabia zilizorithiwa
-Mgandamizo mkubwa wa damu


Sababu nyingine zaweza kuwa;


Kuwa na tatizo la kubahatisha kusimama-watu wenye tatizo la kushindwa kuwa na uimara wa kiungo chao kwa muda mrefu,huwa katika hatari ya kufika kileleni mapema kwa sababu ya hofu ya kupoteza uimara kabla hawajamaliza.

Hofu ama wasiawasi- Wanaume wenye hofu ya kufanya vizuri katika tendo la ndoa au katika mambo mengineyo yoyote,huwa katika hatari ya kutofanya vizuri na kujikuta wanamaliza mapema.

Matatizo katika mahusiano - Kama kuna matatizo kati yako na mwenzi wako ni dhahiri kuwa utakuwa katika hatari ya kutofanya vizuri na kushindwa kabisa kumridhisha mwenzi wako.

Msongo wa mawazo- Msongo wa jambo lolote huondoa utulivu na umakini katika tendo la ndoa na huweza kukusababishia hatari ya kujikuta umefika kileleni haraka.




Tiba ya Kuwahi Kufika Kileleni



Jenga uwezo binafsi wa kuchelewa kufika kileleni haraka- Fanya zoezi la kujichua kidogo na unapoelekea kumwaga acha ,kisha ruhusu zipite kama dakika 5 hivi kisha rudia tena. Fanya hivi kwa mara tatu hadi tano na unaweza kujiruhusu au kutojiruhusu kumwaga baada ya kujichua. Unaweza pia kuchomoa unapohisi unakaribia kumwaga wakati ukiwa na mwenzi wako,kupumzika,kuvuta pumzi nyingi na kupumua taratibu au unaweza kubadili mkao unaokupunguzia hisia kali za utamu ili usifike haraka kileleni.

Tumia kondom- hizi hukupunguzia hisia kali za kufurahia na kukusaidia kuchelewa angalau kufika kileleni, kama utatumia kondom nzito.

Tumia Virutubisho- Virutubisho ni muhimu katika ufanisi wa nguvu za kiume. Kirutubisho kama vile Vig Power kwa mfano, ina uwezo wa kufanya damu nyingi kutiririka kwenye uume na kuupa nguvu ya kushughulika kwa muda mrefu kabla ya kumaliza.





Mazoezi ya kegel- Mazoezi ya kegel husaidia kuongeza uwezo wa mwanaume kuchelewa kumaliza. Utafiti uliofanyika mwaka 2012 ulibaini kuwa wanaume wengi waliokuwa hata hawamalizi dakika moja kabla hawajafika mwisho wa mchezo, walimaliza kozi ya mazoezi haya kwa jumla ya wiki 12, na uwezo wao uliongezeka toka sekunde 32 za mwanzo hadi sekunde 146 baada ya mazoezi.

Jaribu kufanya awamu ya pili- Baada kufika kilelelni kwa haraka na mwenzi wako,jaribu kumliwaza na kumfanya ajisikie vizuri,ili mashine yako ipate moto tena. Ukifanikiwa kuamka tena na kuingia ulingoni, hutafika kileleni haraka kama hapo awali.

Mwandae sana mwenzi wako- Hii ina manufaa kwako kwa sababu utakapokuwa unaingia atakuwa amelainika sawasawa hakutakuwa na msuguano mkubwa. Msuguano mkubwa huongeza hisia kali kwako,na kukusababisha ufikie mwisho haraka.


Inashauriwa pia kuwa ili kupunguza uwezekano wa wewe kumaliza mapema,unaweza kujichua ndani ya masaa 24 kabla ya tendo. Inaweza kufanya kazi maana kw akadri unavyojichua ndivyo unavyopunguza hisia zako za karibu. Lakini pia ikumbukwe kuwa kwa kadri unavyojichua,utazoea kufika mwisho wa safari mapema. Kwa hiyo hii ni sababu inayoweza kujenga na kubomoa hapo hapo



Hiki pia kilikuwa ni kipengele katika tatizo la nguvu za kiume,cha kuwahi kufika kileleni kwa wanaume. Natumai ndugu msomaji umenufaika na elimu iliyotolewa katika mada hii. Mada iliyopita tulitazama  tulitazama tatizo la uume kushindwa kusimama. Katika mada itakayofuata tutatazama tatizo la Kuchelewa kufika kileleni na suluhisho lake. Endelea kufuatana nasi.

Ndugu msomaji kama una tatizo hili na unahitaji kusaidiwa,Wasiliana nasi tutakusaidia. Piga simu 0673 923 959 au tuandikie kupitia maishaniafya@gmail.com.

Pia usiache kutoa maoni yako au kuuliza maswali yako kuhusiana na mada hii. Tunajisikia furaha sana kushirikiana nawe katika mada zetu.


Karibu,