Tatizo la nguvu za kiume limekuwa ni gumzo leo kwa wanaume wengi. Lakini kwa mtazamo wa kina hakuna tatizo ambalo kwa peke yake linaitwa upungufu wa nguvu za kiume. Ila ni mjumuiko wa matatizo yanayochangia mwanaume kushindwa kufanya vema kwenye tendo la ndoa. Mwanaume atashindwa kufanya vema kwenye tendo la ndoa kama atakuwa na tatizo la kushindwa kuwa mwanajeshi imara (Erectile Dysfunction),anawahi kufika kileleni (Premature Enjaculation) ama anachelewa kufika kileleni (delayed enjaculation). Tutaanza kutazama tatizo moja baada ya lingine,ili wewe msomaji wangu upate kuelewa vema tena kwa kina.
Katika mada hii tutalitazama tatizo la jogoo kushindwa kuwika. Huu ni ukosefu wa uwezo wa kiungo cha mwanamume kushindwa kusimama kwa muda wa kutosha ili kumudu kufanya tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa takribani wanaume zaidi ya milioni 30 wanakabiliwa na kusumbuliwa na tatizo hili. Unaweza kuona jinsi tatizo lilivyo hatarishi kwa wanaume wengi. Hili huwa ni tatizo pale utakapojaribu kufanya tendo la ndoa na kupata shida siyo mara moja au mara chache tu, bali kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa kwa kushindwa kusimama kwa uume kwa muda mrefu na jambo hili kuwa endelevu.
Sababu za Jogoo kushindwa kuwika
Kuwika jogoo ni matokeo ya kutiririka damu kwa wingi ndani yake. Hii hutokana na hisia za mapenzi au kuguswa. Mwanaume anapokuwa na hisia za kimapenzi uume hulala. Kulala huku husababisha damu nyingi kujaa katika mishipa yake ya arteri. Damu inapojaa uume husimama na kuwa imara na damu huendelea kuzunguka ndani yake. Kuamshwa kimapenzi kwa mwanamume huhusisha ubongo,homoni,hisia,neva,misuli na mishipa ya damu pia. Tatizo katika mojawapo ya viungo hivyo vinavyohusika husababisha ushindwe kusimama imara kwa ajili ya tendo la ndoa. Wakati mwingine mchanganyiko wa masuala ya kimaisha yanayohusisha magonjwa na changamoto za hapa na pale au masuala ya kisaikolojia yanayohusisha msongo wa mawazo na mengineyo huweza kusababisha tatizo hili. Hebu tuangalie baadhi ya sababu zinazopelekea mwanaume kushindwa kuwa mwanajeshi imara kwenye uwanja wa mapambano.
Sababu za kimaisha
Mara nyingi tatizo la jogoo kushindwa kukwea mlima limekuwa likisababishwa na sababu nyingi za kimaisha. Sababu hizo zaweza kuwa;
-Magonjwa ya moyo kama vile heart attack, heart failure na angina pectoris.
-Kufinyika kwa mishipa ya damu (Atherosclerosis)
-Mgandamizo mkubwa wa damu (High blood presssure)
-Cholestrol nyingi
-Kisukari
-Unene uliopitiliza
-Metabolic syndrome-Ni hali inayohusisha mgandamizo mkubwa wa damu,kiwango cha juu cha insulin,mafuta mengi maeneo ya kiunoni na cholesterol nyingi.
-Matumizi ya sigara-Kukosa usingizi vizuri
-Kunywa pombe kwa wingi
-Makovu kwenye uume
-Matatizo ya tezi dume na tiba yake
-Ajali ya uti wa mgongo
-Kiwango kidogo cha homoni ya Testesterone
-Matumizi ya madawa kama vile,madawa ya kuzuia mfadhaiko,high blood pressure na za kuzuia maumivu.
Sababu za kisaikolojia
Ubongo hufanya kazi kubwa katika kuamsha mfululizo wa matukio yanayopelekea uume kusimama. Lakini kuna mambo mengi yawezayo kuchangia kuhafifisha utendaji kazi wa ubongo na hivyo kusababisha tatizo la jogoo kushindwa kukwea mlima. Mambo hayo ni kama yafuatayo;
-Mfadhaiko
-Hofu
-Msongo wa mawazo
-Mawasiliano mabaya yasababishayo mahusiano mabaya baina ya wenzi
Jinsi ya kudhibiti na kutibu tatizo la jogoo kushindwa kuwika
Hatua hizi hufanikiwa kupitia mambo kadha wa kadha. Mambo haya huweza kuwa,Mfumo wa maisha na kudhibiti magonjwa mbalimbali na kuongeza homoni. Hebu tutazame hatua hizo.
Mfumo wa maisha- Baadhi ya mambo ya kila siku ya namna unavyoishi huweza kuchangia sana katika tatizo la jogoo wako kushindwa kuwika. Kuyaepuka husaidia kuimarisha uwezo wa uume wako kusimama imara kwa muda mrefu. Mambo hayo ni kama yafuatayo;
Epuka uvutaji wa sigara-uvutaji wa sigara kwa kawaida husababisha mishipa ya damu kusinyaa na kusababisha damu kupita kwa shida. Hii ndiyo hupelekea damu kutofikishwa vyeme kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume.
Punguza uzito wako-Uzito uliopitiliza husababisha tatizo la high blood pressure ambalo pia ni miongoni mwa sababu hatarishi za jogoo kushindwa kupanda mlima.
Fanya mazoezi- mazoezi husababisha mzunguko wa damu kuwa katika hali nzuri,jambo lililo muhimu kwa ajili ya kuuwezesha uume kusimama na kuongeza nguvu zako.
Epuka kunywa pombe- madhara ya pombe kwa mwanamume ni kama ilivyo kwenye uvutaji wa sigara ambao unadhoofisha kabisa ufanyaji kazi wa mishipa ya damu kuleta damu kwenye viungo vya uzazi.
Imarisha mahusiano na mwenzi wako-mahusiano yaliyoimarishwa huboresha hisia za ukaribu baina ya wenzi,na kuboresha ufanisi wa tendo la ndoa.
Epuka msongo wa mawazo- msongo wa mawazo ni chanzo kikubwa cha jogoo kushindwa kuwika. Msongo wa mawazo unahatarisha sana ufanisi wa wanaume katika ufanyaji wa tendo la ndoa kwa sababu huweza kusababisha tatizo la high blood pressure na kisukari.
Lakini pia magonjwa haya yakidhibitiwa tatizo litapungua kwa kiwango kikubwa;
High blood pressure- mgandamizo mkubwa wa damu hutokana na mishipa ya damu kujifinya na kuwa myembamba,hali inapelekea nguvu ya kusukuma damu kuongezeka. Hii huweza kusababisha mishipa kupasuka,na damu kushindwa kufika kwenye mishipa ya uume wako,na hivyo tatizo la kushindwa kusimama kwa muda mrefu hutokea.
Kisukari- sukari ikizidi mwilini husababisha huyu mwanaume ashindwe kuwa mwanajeshi imara.
Cholestrol- Kuzidi kwa cholestrol husababisha tatizo la kupungua kwa upana wa mishipa ya damu (atherosclerosis),na pengine huweza kupelekea mishipa ya damu kuziba,na kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Homoni ya testesterone- homoni hii huongeza hamu ya tendo la ndoa na mbegu za kiume. Homoni hii huzalishwa ndani ya korodani za mwanaume. Kuepuka matumizi ya dawa zinazohafifisha utengenezwaji wa homoni hii,kutaongeza uwezo wa uume wako kusimama kwa muda mrefu. Madawa hayo ni kama ya madawa ya kpunguza mfadhaiko na pressure.
Tumetazama kwa undani upungufu wa nguvu za kiume katika kipengele cha uume kushindwa kusimama. Mada itakayofuata tutazama tatizo la kuwahi kufika kileleni na tatizo la kuchelewa kufika kileleni pia. Endelea kufuatana nasi ndugu msomaji wangu.
Je,una tatizo la kushindwa kuwa mwanajeshi imara kwenye uwanja wa mapambano? Je,huwezi kukwea mlima vema? Tuna suluhisho kwa ajili yako,Wasiliana nasi kwa barua pepe maishaniafya@gmail.com au piga simu 0673 923 959.
Ukiwa na swali,maoni au ushauri kuhusiana na mada hii, tafadhali wasiliana nasi kupitia kisanduku cha maoni hapo chini.


