HOMA YA INI - HEPATITIS C

Hepatitis C ni ugonjwa wa ini unaosababishwa na maambukizi ya virusi. Hepatitis c husababisha maambukizi kwenye ini,ambayo huweza kusab... thumbnail 1 summary



Hepatitis C ni ugonjwa wa ini unaosababishwa na maambukizi ya virusi. Hepatitis c husababisha maambukizi kwenye ini,ambayo huweza kusababisha ini kuharibika kabisa. Hepatitis c husababishwa na virusi wa hepatitis c (HCV) ambao huenezwa kwa njia ya damu iliyochafuliwa.

Virus wanaosababisha hepatits c huleta madhara taratibu sana. Unaweza kujisikia mzima na huumwi kwa kipindi cha miaka kadhaa.Katika kipindi chamiezi 6 hadi 12 ya mwanzo baadhi huweza kujisikia vibaya,kama wanahisi dalili za mafua hivi.

Ni katika kipindi hiki,kinga za mwili huanza kupambana na virusi wa HCV. Mtu mmoja katika watu 4,mfumo wa kinga huweza kuondosha virusi kabisa,lakini kwa walio wengi huhitaji tiba na kama tiba haijatolewa mapema,husababisha maambukizi ya kudumu yanayoweza kupelekea madhara ya kudumu kwenye ini.



Dalili Za Ugonjwa Wa Hepatitis C



Dalili za hepatitis c huweza kuonekana baada ya virusi wa hepatitis c kusababisha madhara zaidi kwenye ini. Baadhi ya dalili hizo ni kama:

-Kutokwa damu kwa haraka

-Ngozi kuvilia damu kwaharaka

-Njano (ngozi,macho kuwa ya njano)

-Maumivu ya tumbo

-Kupoteza hamu ya chakula

-Kichefuchefu

-Uchovu

-Miwasho kwenye ngozi

-Tumbo kujaa maji

-Miguu kujaa

-Uzito kupungua

-Mishipa ya damu ndani ya ngozi kuonekana kama nyuzi za buibui

-Kuchanganyikiwa na kukosa utulivu



Chanzo Cha Homa Ya Hepatitis C




Chanzo cha homa ya hepatitis c ni virusi wa hepatitis c (HCV). Maambukizi huenea pale damu iliyoambukizwa virusi hawa inapochanganyika na damu ya mtu asiye na maambukizi.

 Mambo Yanayochangia  Hepatitis C Kuenea:

-Kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vyembe na sindano

-Kuchangia vifaa vya kujidungia madawa

-Kufanya mapenzi na mtu aliyeathirika

-Kuchora tatoo na kuchomwa na vitu vyenye ncha kali alivyotumia mwathirika

-Kunyonyesha japo ni nadra sana kutokea

-Maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua



Nani Wako Katika Hatari Ya Kuambukizwa Hepatitis C?



Watu walio katika hatari ya kuambukizwa hepatitis c ni hawa wafuatao:

-Watu wanaoongezwa damu kutoka kwa mtu aliyeathirika

-Waliowahi kujidunga sindano

-Aliyewahi kuongezwa damu au kubadilishiwa kiungo ndani ya mwili kabla ya mwaka 1992

-Waliozaliwa kati ya miaka 1945 na 1965

-Waliofanyiwa uangalizi wa figo

-Wenye maambukizi ya VVU

-Waliozaliwa na mama mwenye maambukizi ya hepatitis C


Madhara Ya Homa Ya Hepatitis C


Ini kuharibika-kama mgonjwa atakaa na ugonjwa kwa miaka takribani 20 hadi 30 anaweza kupata tatizo la ini kuharibika (cirrhosis)

Saratani ya ini-baadhi ya watu wenye maambukizi ya hepatits c virus huweza kupata kansa ya ini

Ini kushindwa-hii ni hatua ya mwisho ya ini kuharibika kabisa

Unaweza kujikinga na maambukizi ya virus wanaosababisha hepatitis c,epuka matumizi ya vitu vyenye ncha kali na watu wengine,jiepushe na ngono isiyo salama na kuwa na wapenzi wengi pia. Lakini unaweza kuzuia madhara yatokanayo na hepatitis c kwa kupata tiba ya hepatitis c mapema.

Kupata dawa na bidhaa tiba za kusaidia kuepuka madhara hepatitis c,wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie kupitia +255 673 923 959.


No comments

Post a Comment