Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ni tatizo linalowapata wanawake wengi kuliko wanaume. Tofauti na wanaume ambao ni asilimia ndogo tu takribani 23 walio radhi kuisha na tatizo hili, asilimia kubwa ya wanawake takribani 46 wako radhi kuendelea kuishi na tatizo hili.
Tatizo la wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa mara nyingi huchangiwa na mambo mengi. Miongoni mwa mambo hayo huweza kuwa mahusiano mabaya baina yako na mwenzi wako,changamoto za maisha na kuchoka sana, historia ya mahusiano yaliyopita, ujauzito,kukoma hedhi ama ugonjwa.
Huna sababu ya kuendelea kuishi na tatizo hili,maana yapo mambo mengi unayotakiwa kufanya ili uondokane na tatizo hili. Kwanza kubali kuwa una tatizo,halafu fanya mambo kadhaa yatakayokusaidia kuondokana na tatizo hili na pia tumia baadhi ya dawa ili kuondokana na tatizo hili.
Kwa Nini Mwanamke Anakosa hamu ya tendo la ndoa?
1.Sababu za kimaisha
Maumivu katika kufanya tendo la ndoa- Mwanamke akiwa anpata maumivu wakati wa tendo la ndoa ama hafiki kileleni wakati wa tendo la ndoa,huweza kukosa kabisa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Mtindo wa maisha-Kutumia pombe kwa wingi,kuvuta sigara na matumizi ya madawa ya kulevya husababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Upasuaji-Upasuaji uliofanyika maeneo ya via vya uzazi ama maeneo ya maziwa hubadilisha mwonekano wa mwanamke,ufanyaji kazi wa viungo vyake vya uzazi na kumsababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Uchovu-Uchovu unaotokana na kuihudumia familia (watoto au wazee) huweza kumsababisha mwanamke kukosa hamu ya mapenzi pia.
Matumizi ya madawa-Matumizi ya madawa ya kuondoa mfadhaiko ama msongo wa mawazo,huweza kuondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.
Magonjwa-Baadhi ya magonjwa humwondolea mwanamke hamu ya tendo la ndoa. Magonjwa ya maungio ya mifupa-Arthritis,kansa,kisukari,high blood pressure,magonjwa ya mishipa ya damu na magonjwa ya fahamu huweza kumwondolea mwanamke hamu ya kufanya tendo la ndoa.
2. Mabadiliko ya mfumo wa homoni
Mabadiliko katika mfumo wa homoni huweza kuathiri hamu yako ya tendo la ndoa. Mabadiliko hayo yaweza kuwa;
Kukoma hedhi-Mwanamke anapoelekea wakati wa kukoma hedhi kiwango cha homoni ya oestrogen hupungua. Hii husababisha mwanamke kupoteza hamu ya kufanya mapenzi. Kupungua kwa oestrogen pia husababisha ukavu wa nyeti za mwanamke. Hii hupelekea mwanamke kujisikia maumivu makali wakati wa tendo na hamu ya kufanya mapenzi hupotea.
Katika wakati huu pia mwanamke huwa na upungufu wa homoni ya testesterone ambayo huongeza hamu ya mapenzi kwa mwanamke na mwanamme. Japo wanawake wengi huendeleaa kuwa na hamu hata baada ya kukoma hedhi,baadhi yao hupungukiwa na hamu kutokana na kupungukiwa na homoni hizi.
Ujauzito na kunyonyesha-Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito,usumbufu wa mimba,kunyonyesha na kumhudumia mtoto huweza kuathiri hamu ya tendo la ndo kwa mwanamke.
3.Matatizo ya kisaikolojia
Yapo matatizo mengi ya kisaikolojia yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa.Matatizo hayo yaweza kuwa;
-Wasiwasi,msongo wa mawazo na mfadhaiko
- Mawazo dhidi ya fadha na masuala ya kazi.
-Kutojithamini
-Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi
-Kuwa na historia mbaya-kunyanyaswa,kubakwa.
4. Mahusiano baina ya wenzi
Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kiungo cha kwanza katika kujenga mapenzi yake na mwanamme. Hivyo tatizo lolote katika mahusiano yenu laweza kuleta athari katika hamu ya tendo la ndoa. Mara nyingi kukosa hamu huweza kutokana uwepo wa mambo yanayoendelea kwa muda mrefu kama haya;
-Kukosekana kwa mawasiliano baina yako na mwenzi wako
-Kupigana ama migogoro isiyokwisha ama kusuluhishwa kwa muda mrefu
-Kukosekana kwa uaminifu katika mahusiano yenu
-Mwanamme kutotambua ama kutomfanyia mwanamke kile anachotaka katika mapenzi-(mwanamke anahitaji kupendwa kwa maana yake ya kupendwa)
Dalili za kukosa hamu ya tendo la ndoa
Hakuna dalali za moja kwa moja kuelezea kukosa hamu ya kufanya mapenzi,isipokuwa hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine. Kwa kawaida kama umekuwa hujisikii kufanya tendo la ndoa kwa sasa kuliko ilivyokuwa hapo kwanza tunaweza kusema,hamu yako imepungua. Ukikuta mwenzi anakuwazia ama anakuhitaji,lakini wewe kwa muda mrefu hata hujisikii kumhitaji inawezakuwa ni viashiria vya awali kukujulisha kuwa unaweza kuwa na tatizo. Dalili zingine pia zaweza kuwa kukosa kabisa hisia zozote za kimapenzi unapokuwa na mwenzi wako,kuwa huru na kujihisi huhitaji kabisa kukutana na mwenzi wako na furaha yako ni kukaa mbali kwa msemo wa mtaani kulala mzungu wa nne.
Jinsi ya kuondoa tatizo la kukosa Hamu ya kufanya tendo la ndoa
Kuna baadhi ya mambo yakifanyika huweza kumsaidia mwanamke kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Mambo yafuatayo ni muhimu kufanyika ili kuboresha hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.
Kufanya mazoezi-Mazoezi ya kuongeza pumzi na nguvu huweza kuongeza stamina na kuboresha mwonekano wako wa mwili na ufanisi wa mzunguko wa damu.
Punguza msongo wa mawazo-Jitahidi kuepuka mawazo mazito dhidi ya masuala yako ya kifedha na kazi na hapo utakuza hamu yako ya kufanya tendo lako la ndoa.
Wasiliana na mwenzi wako-Wenzi waliojifunza kuwasiliana kwa uwazi na ukweli hufanikiwa kuimarisha mahusiano yao. Kuzungumza juu ya mahusiano yenu,mambo mnayopenda na msiyopenda pia huboresha mahusiano yenu na kuboresha tendo la ndoa.
Boresha ukaribu wako na mme wako-Ukaribu wenu utarudisha hamu na hisia zilizokuwa zimetoweka kwa muda mrefu.
Rekebisha mtindo wako wa maisha-Acha kuvuta sigara,kutumia madawa ya kulevya na pombe ili hali yako ya uimara na kuvutiwa na kuwa karibu na mwenzi wako iimarike.
Chakula kinachoweza kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
1.Parachichi
Parachichi ina mafuta (fats),madini na vitamini B6 ambazo huongeza nishati na hamu ya kufanya tendo la ndoa
2. Strawberries
Strawberries ina antioxidants inayosaidia afya ya mishipa ya damu (arteries) na moyo inayosafirisha damu kwenye mishipa ya damu na kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa.
3.Almonds
Hizi zina nadimi ya zinc,selenium na vitamon E,ambazo ni muhimu katika kuboresha afya ya tendo la ndoa.
4.Asparagons
Vitamin B6 na folic acid inayopatikana humu, huongeza hamu sana na kumfanya mwanamke aweze kufika kileleni vizuri
5. Tikitimaji
Ina lycopene na phytonutrients ambazo hufanya mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri,na kufanya damu izunguke vyema na kufika sehemu maalumu zinazotakiwa. Mzunguko wa damu kwenye misipa ya damu,huleta ufanisi katika tendo la ndoa.
6. Viazi vitamu
Vina potasium ambayo husaidia kuondoa tatizo la high blood pressure ambayo pia ingeweza kupunguza ufanisi wa tendo la ndoa.
Vyakula vingine vitakavyokusaidia ni samaki wenye mafuta,kahawa,chai,ndizi na tangawizi.
Je, una tatizo hili au je, mahusiano yako yameyumba kwa sababu ya tatizo hili? Usiwaze sasa na kukosa amani maana linatibika kabisa. Wasiliana nasi kwa njia iliyo rahisi kwako katika zilizoorodheshwa hapo chini.
Kwa maoni,msaada ama swali lolote,tafadhali wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie 0673 923 959.



