UGUMBA KWA MWANAMKE-ZIJUE SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA MTOTO

Ugumba ni hali ya mwanamke kukosa uwezo wa kupata mtoto. Mwanamke atasemekana kuwa ni mgumba pale atakapokutana na mwenzi wake katika ... thumbnail 1 summary






Ugumba ni hali ya mwanamke kukosa uwezo wa kupata mtoto. Mwanamke atasemekana kuwa ni mgumba pale atakapokutana na mwenzi wake katika siku zake za hatari bila kinga,na asiweze kupata mimba kwa takribani miezi 12. Uwezo wa mwanamke kushika mimba hupungua kadri umri wake unavyoongezeka. Kuanzia miaka 35 na kuendelea,wanawake walio wengi hushindwa kupata ujauzito hadi miezi 6,na hili kwao ni kawaida. Lakini ikizidi miezi 6 hapo huwa ni tatizo,na wenzi hao hutakiwa kupata ushauri kwa watalaam. Tafiti zimeonesha kuwa zaidi ya 50% ya matatizo yote ya ugumba hutokana na matatizo ya wanawake na wakati kama 20% hivi ndio huchangiwa na wanaume,wakati 30% huchangiwa nao wote.

Kuna aina mbili za ugumba,Aina hizo ni;

Primary Infertility- Ni hali ya wenzi ambao hawajawahi kupata mtoto kukosa mtoto kwa takribani miezi 12 hivi ya kushiriki pamoja bila kinga.

Secondary Infertility- Ni hali ya wenzi kushindwa kupata mtoto mwingine kwa muda mrefu baada ya kupata angalau mtoto mmoja.

Ili kuelewa vyema tatizo hili,hebu tazama mfumo wa uzazi wa mwanamke ulivyo;








.Ovary- huzalisha mayai ya kike.
.Fallopian tubes- husafirisha mayai toka kwenye ovari na kufikia mfuko wa mimba. Hapa ndipo yai la kike linaporutubishwa na mbegu ya kiume.
.Uterus- hushikiza yai lililorutubishwa kwenye mirija ya fallopia
.Cervix- ni shingo ya kizazi. Hii hutoa ute unaosaidia kusafirisha mbegu za kiume kulifikia yai la kike ili kulirutubisha.


Ugumba kwa mwanamke hutokea endapo;

-Yai lililojishikiza kwenye kuta za uterus kushindwa kuendelea kuishi
-Yai lililorutubishwa kushindwa kujishikiza kwenye mfuko wa uzazi ( uterus)
-Mayai yaliyozalishwa na ovari kushindwa kufika kwenye mfuko wa mimba na hivyo kushindwa kurutubishwa.
-Ovari kushindwa kuzalisha mayai.




Sababu za Mwanamke Kukosa Mtoto





Matatizo ya kutokomaa kwa yai ( Ovulation Disorders)- Tafiti zimeonesha kuwa matatizo ya kushindwa kukomaa na kuachiwa kwa yai ni sababu kubwa cha ugumba kwa wanawake. Kila mwezi yai moja (kwa bahati yaweza kuwa zaidi ya moja) hukomazwa na kuachiwa toka kwenye ovari ili lirutubishwe. Katika hali isiyo ya kawaida kwa,inawezekana mayai yakashindwa kukomaa kabisa na wakati mwingine inaweza kutokea kwa mwezi husika. Matatizo haya ya kushindwa kukomaza mayai huweza kutokana na mambo yafuatayo;

-Ovari kushindwa kufanya kazi vizuri mwanamke akiwa hajafikisha miaka 40
-Kuzalishwa kwa homoni ya prolactin kwa wingi wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi. (Prolactin ni homoni inayoongeza maziwa kwa mama mjamzito ama anaenyonyesha).
-Kuzalishwa mayai dhaifu. Hii mara nyingi huwapata akina mama wenye umri mkubwa.
-Homoni ya thyroid kuzalishwa kwa wingi na kusababisha matatizo katka ovulation
-Homoni ya thyroid kutengenezwa kwa kiwango kidogo na kusababisha pia matatizo ya ovulation

Kukoma Hedhi mapema- kukoma hedhi mapema ni tatizo ambalo bado halijajulikana chanzo chake hadi sasa. Kuna baadhi hukoma haraka na wengine huchukua muda mrefu kukoma hedhi. Mwanamke kukoma hedhi ni sababu tosha ya kushindwa kupata mtoto kabisa.

Endometriosis- Ni hali ambapo tishu zinazojenga kuta za uterus huacha kujenga uterus na kuanza kujenga sehemu nyingine kama vile kwenye ovari. Hii huharibu ovari na mirija ya fallopia na kusababisha mwanamke kukosa uwezo wa kupata mtoto.

Pelvic Inflammatory Diseases (PID)- Ni maambukizi yanayoanzia kwenye mfuko wa uzazi ( uterus) na kuenea sehemu nyingine zikiwemo mirija ya fallopia na ovari. Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa. Maambukizi haya huweza kusababisha mirija ya fallopia kuziba na kuikosesha uwezo wa kusafirisha yai kutoka kwenye ovari. Hii ina maana kwamba yai halitaweza kurutubishwa ndani ya mirija ya falopia jambo linalomkosesha mwanamke uwezo wa kushika mimba.

Fibroids- Ni uvimbe usio wa kansa ndani ya mfuko wa uzazi. Uvimbe huu kwa namna moja ama nyingine huweza kuzia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye mfuko wa uzazi (uterus). Fibroids hizi pia huweza kuziba mirija ya falopia na kusababisha hitilafu katika suala zima la kutungwa mimba.

Upasuaji-upasuaji maeneo ya chini ya tumbo (nyonga) ,huweza kusababisha hitilafu kwenye mirija ya fallopia inayounganisha mfuko wa mimba na ovari. Pia upasuaji kwenye shingo ya kizazi (cervix) huweza kufupisha shingo ya kizazi na kusababisha matatizo kwenye mfuko wa uzazi.


Matatizo ya ute-Mbegu za mwanamume huweza kuogelea na kulifikia yai ili kulirutubisha kwa msaada wa ute unaotolewa na shingo ya kizazi. Kama kutakuwa na matatizo ya ute kutolewa ama kutengenezwa,itakuwa na vigumu sana kushika mimba.

Madhara yatokanayo na madawa- Baadhi ya madawa huweza kuhafifisha uwezo wa mwanamke kupata mtoto. Madawa hayo ni kama yafuatayo;

            .Non-Steroidal Anti-Inflammatory Drugs (NSAIDs)-hizi ni dawa za kupunguza                maumivukama vile ibprofen ,aspirin au diclofenac. Matumizi ya dawa hizi kwa muda mrefu,husababisha mwanamke kushindwa kupata ujauzito baadae.

             .Chemotherapy- Ni madawa wanayotumia watu wenye matatizo ya kansa. Matumizi ya dawa hizi huweza kusababisha ovari kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha.

             .Neuropletic Medicines- Ni dawa zinazotumika kutibu tatizo la akili kupumbaa (psychosis). Dawa hizi husababisha miezi mingine kupita bila kuziona siku zako ama huweza kusababisha ugumba kabisa.

              .Spironolactone- Ni dawa inayotumiwa na wagonjwa wenye tatizo la miguu kujaa maji (Oedema). Matumizi ya dawa hii husababisha ukosefu wa kizazi kwa mwanamke,lakini akiacha kutumia dawa hii baada ya miezi miwili uwezo wa kupata mtoto hurejea.

Magonjwa- Magonjwa ya muda mrefu kama vile Kansa na UKIMWI huweza kusababisha matatizo katika ukomavu wa yai.



Mambo yanayoweza kuhatarisha Mwanamke ashindwe kupata Mtoto










Matumizi ya madawa ya kulevya- madawa ya kulevya kama vile marijuana na cocaine,husababisha hitilafu kwenye mfumo wa uzazi na mwanamke kushindwa kuzaa kabisa.

Mazoezi- Kufanya mazoezi kwa kiwango kidogo,husababisha tatizo la unene,jambo linalochangia kukosa uwezo wa mwanamke kushika mimba. Wakati huo huo kufanya mazoezi kupita kiasi (zaidi ya masaa 7 kwa wiki) husababisha matatizo ya ovulation kwa mwana

Uzito mkubwa kupita kiasi- kuwa na uzito mkubwa sana huweza kusababisha mwanamke kushindwa kupata ujauzito.

Kuwa na uzito mdogo- Wanawake walio katika hatari ya kukosa watoto ni wale wasiokula vizuri. Kutokula kutakusababisha kupungua uzito wako sana jambo linalokusesha uwezo wa kuzaa.

Matumizi ya pombe- Kwa mwanamke yeyote asiyetaka kukosa kupata mtoto, ni lazima akubali tu kuacha pombe. Kunywa pombe nyingi kutapunguza uwezo wa kushika mimba kwa mwanamke.

Kuvuta sigara- Uvutaji wa sigara iwe tumbaku au aina yoyote ya madawa,huchangia mwanamke kukosa kizazi. Mimba nyingi htoka kama mama huyu atakuwa ni mvutaji. Pia hupunguza ufanisi wa tiba ya kukosa kizazi kama unatumia huku unavuta.

Umri- kukosa uwezo wa kuzaa huendana na umri pia. Kuanzia miaka 30 uwezo wa kuzaa huanza kupungua na tatizo huwa kubwa baada ya miaka 37. Ugumba kwa akina mama wenye umri mkubwa huchangiwa na idadi na ubora wa mayai yake.

Msongo wa mawazo- Tafiti zimeonesha kuwa,msongo wa mawazo huchangia kwa kiwango kikubwa kwa mwanamke kukosa uwezo wa kushika ujauzito. Msongo hupunguza hamu ya tendo la ndoa na hivyo kusababisha mwanamke kukosa uwezo wa kupata mtoto.

Maambukizi ya zinaa- husababisha mirija ya falopia kuziba na kuzuia yai kurutubishwa na mbegu ya mwanamume,jambo linalosababisha mwanamke kushindwa kupata mtoto.

Kemikali katika mazingira- Tafiti zimebaini uwepo wa kemikali kadha wa kadha zinazosababisha mwanamke kukosa watoto. Kemikali hizo ni kama zifuatazo;

     .Mionzi- tiba za mionzi ya mara kwa mara huathiri utendaji kazi wa ovari.

     .Lead- Husababisha mimba kutoka

      .Ethylene Oxide- Ni kemikali inayotumika kuua wadudu katika vifaa vya kufanyia upasuaji.                                      Lakini pia hutengeneza dawa ya kuulia wadudu. Hii husababisha dosari katika                                       mimba changa na kusababisha mimba kutoka.

     .Dibromochloropropane (DBCP)- Ni kemikali inayopatikana katika dawa ya kuulia wadudu. Hii                                       husababisha mwanamke kukoma hedhi mapema.



Akina mama wengi wanahangaika sana kutafuta watoto. Kuna jambo napenda nikushauri kidogo hapa. Kabla hujafikiria njia gani utumie kupata mtoto,tafuta kwanza chanzo cha tatizo lako. Kama tatizo ni mvurugiko wa homoni,ninakuhakikishia kuwa unaweza kupata mtoto haraka. Dawa zetu zina uwezo wa kuweka homoni zako katika msawazo mzuri,nawe utapata mtoto na kuondokana na tatizo la ugumba ikiwa linakusumbua. Kama tatizo ni mirija ya falopia kuziba tafadhali pokea ushauri wa kitabibu toka kwa daktari wako.


Tumekuwa na mada ndefu sana juu ya sababu za mwanamke kukosa mtoto. Naamini umenufaika na mada hii na kujifunza mengi.Katika mfululizo huu tumetazama mzunguko wa hedhi, Maumivu kabla ya Hedhi, Maumivu baada ya Hedhi na Sababu za mwanamke kukosa Hamu ya tendo la ndoa. Usiache kuungana nasi katika mada zitakazofuata.

Kwa msaada wa karibu,maoni ama maswali kuhusiana na mada hii,tafadhali wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com ama simu  0673 923 959.